KURUGENZI
ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, imesema Rais Jakaya Kikwete hana mamlaka
ya kusitisha Bunge Maalumu la Katiba kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko
ya Katiba.Mkurugenzi
wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu, Bw.Salva Rweyemamu, aliyasema hayo
Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Bw.
Rweyemamu alikuwa akikanusha taarifa iliyoandikwa na gazeti moja
linalotoka mara moja kwa wiki ambalo liliandika habari iliyobeba kichwa
cha habari “Rais Baraka Obama amgeuka JK”.
Aliongeza
kuwa, sheria hiyo haitoi nafasi kwa mtu mwingine kulivunja Bunge hilo
bali tofauti zilizopo watazimaliza wenyewe akiwataka wajumbe wa Bunge
hilo waliosusia vikao kutoka kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA), warejee bungeni kuendelea na vikao ili wananchi wapate Katiba
Mpya.
Akizungumzia
taarifa iliyoandikwa na gazeti hilo, alisema habari hiyo haina ukweli
bali imetungwa kwani katika mkutano uliofanyika Mjini Washington D.C,
nchini Marekani hivi karibuni, masuala hayo hayajazungumzwa kama
inavyodaiwa.
alisema.
Alisema
katika mkutano uliowakutanisha viongozi mbalimbali, hakuna jambo la
IPTL ambalo lilizungumzwa ambapo Rais Kikwete alikutana na Mtendaji Mkuu
wa Shirika la Misaada la Maendeleo nchini Marekani la Millennium
Challenge Corporation (MCC) na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Aliongeza
kuwa, Rais Kikwete pia alizungumza na Rais wa Malawi, Peter Mutharika
ambaye alimkaribisha nchini kwake ili wakale samaki wa ziwa Malawi
linalojulikana kama ziwa Nyasa
Post a Comment