|
Mbunge Filikunjembe na Mafulu wakipongezwa kwa kuteuliwa walezi wa UWT Njombe |
Dr Suzana Kolimba wa tatu kushoto akipongezwa kwa mchango wake UWT |
walezi wa UWT mkoa wa NJombe mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe ( kulia ) na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Lediana Mafulu wakipongezana kwa kuteuliwa kuwa walezi wa UWT mkoa wa Njombe |
Wabunge Filikunjombe na Lediana wakiwa katika pozi
Na Mathias Canal, Kwanza Jamii-Ludewa
Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mkoani Njombe Deo Filikunjombe, pamoja na Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Iringa Lediana mafulu Mng’ong’o, wamesimikwa kuwa walezi wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoani Njombe.
Sawia na kusimikwa kuwa walezi wa UWT mkoa wa Njombe pia Mbunge wa viti maalum Mkoani Njombe Pindi Chana amewakabidhi Katiba ya jumuiya ya Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT) ya mwaka 1978.
Akitoa shukrani kwa kuteuliwa kuwa mlezi wa UWT Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Iringa Lediana mafulu Mng’ong’o, amesema kuwa ameanza kufanya kazi na wanawake tangu mwaka 1982 hivyo ana uzoefu na ataitendea haki kazi aliyopewa pasipo kukiuka katiba ya UWT.
Hata hivyo Mng’ong’o amesema amefanya kazi na Deo Filikunjombe miaka mitano, hivyo amempongeza kwa kuteuliwa kuwa Mlezi wa UWT na kuahidi kushirikiana naye bega kwa bega ili kufanikisha adhma ya Wajumbe walio muamini na kumteua.
Kwa upande wake rafiki wa mbunge wa Ludewa ambaye yeye ni mbunge wa Mwibala Wilayani Bunda Kangi Lugola, amempongeza Rafiki yake Deo Filikunjombe kwa kuwa mlezi wa UWT kwa kusema kuwa ni kiongozi makini na daima hutambua kile anachokifanya.
Amesema kumteua kwao kuwa mlezi wao wamefanya jambo la msingi kwani wataweza kusonga mbele katika umoja wao tofauti na angechaguliwa mbunge mwingine ambaye ni kiroho papo (hathamini shughuli za wanawake).
Lugola Ameahidi kufanya semina na Wajumbe wa CWT Mkoani Njombe kwa ajili ya Oparesheni Ondoa michepuko (Oparesheni Ondoa wapinzani) ambayo wapo kwenye Mkoa wa Njombe.
Kwa upande wake Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe, AKizungumza na wajumbe baada ya kusimikwa kuwa mlezi wa UWT Mbunge wa amewashukuru wajumbe hao kwa kuwa na imani naye na kusema kuwa anatambua mchango wa wanawake hapa Tanzania hivyo alipopata taarifa ya kuombwa kuwa mlezi hakusita kukubali.
"Si kazi ndogo kumuongoza mama ambaye amekuzaa, na kukulea hatimaye anabadilika na kukutaka kumlea, hakika ni jambo ambalo linahitaji hekima na ujasiri mkubwa sana" Alisema Filikunjombe.
Amesema kuwa atashirikiana na wajumbe wote ili kuhakikisha UWT mkoa wa Njombe inakuwa na kuleta heshima kubwa hapa nchini Tanzania na nje ya nchi.
Sawia na hayo aliendesha harambee ya kuchangia gari kwa ajili ya kuwatembelea wajumbe waishio maeneo ya mbali ili kuweza kurahisisha shughuli za maendeleo ya UWT.
Katika harambee hiyo zilipatikana jumla ya fedha shilingi 15,000,000, hivyo kufikia idadi ya shilingi 21,000,000 sambamba na fedha shilingi 6,000,000 ambazo zilikuwepo kwenye mfuko wa UWT kabla ya harambee hiyo.
“Imani kubwa mliyoionyesha kwangu hii leo na mnayoendelea kuionyesha kwangu mimi, naitambua na kuithamini hivyo lazima nifanye kazi kwa ufasaha ili UWT mkoa wa Njombe iweze kukua, kudumu na kuwa ya kihistoria” Alisema Filikunjombe
Post a Comment