Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MANCHESTER UNITED WATENGA PAUNI MILIONI 100 KWA DI MARIA

                                      


Angel Di Maria.
KLABU ya Manchester United imetenga kitita cha pauni milioni 100 kwa ajili ya usajili na mshahara wa winga wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Argentina, Angel Di Maria.

Daley Blind.
Pauni milioni 50 zinatarajiwa kutumika kumsajili staa huyo wa Real Madrid huku mshahara wake kwa wiki ukitarajiwa kuwa pauni 200,000.
Kocha wa United, Louis van Gaal amemtaka Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Ed Woodward kumsajili Di Maria kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Marcos Rojo.
Maamuzi hayo yamekuja baada ya timu hiyo kuanza vibaya Ligi Kuu ya England 'Premiership' kwa kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Swansea juzi Jumamosi.
Mbali na Di Maria, United pia wanawawinda wachezaji Daley Blind wa Ajax na Marcos Rojo kutoka Sporting Lisbon.GPL. (P.T)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top