Serikali
imesema ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya fedha za malipo ya
mafunzo kwa vitendo kwa mwaka wa masomo 2013 2014.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano Cosmas
Mwaisobwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam.(Martha Magessa)
Mwaisobwa
alisema kuwa jumla ya wanafunzi 9946 kutoka vyuo vikuu vitano
hawajapatiwa fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo ambao wengi wao
tayari wako katika maeneo waliyopangiwa.
"Bodi
tayari imeandaa malipo yao na yanatarajiwa kutumwa mwishoni mwa juma
hili, ambapo vyuo vikuu vitano ikiwemo Tumaini Makumira (TUMA) wanafunzi
1 715, Stefano Moshi (SMMUCO) wanafunzi 1 191, Chuo Cha Usimamizi wa
Fedha (IFM)wanafunzi 2 578, Mt. Augustino (SAUT) wanafunzi 2639 na
Teofilo Kisanji (TEKU) wanafunzi 1823.
Akijibu
swali la waandishi wa Habari Mwaisobwa alisema kuwa sababu zilizopelekea
kuchelewa kwa fedha hizo ni mchakato wa upatikanaji wa fedha
zilitarajiwa kupatikana mapema zaidi.
Aidha,
Mwaisobwa alitoa rai kwa wazazi na walezi wenye uwezo wa kuwalipia
watoto wao wafanye hivyo ili kuwapa nafasi wale wasio na uwezo wa
kunufaika na mkopo mkopo wa Bodi.
Post a Comment