Mkazi
wa Kijiji cha Bupu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Forodesi Ntabegera
(30) ameuawa kwa kubakwa, kisha kunyongwa na watu wasiojulikana, kisha
mwili wake kutupwa kichakani.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Athuman Mwambalaswa alieleza kuwa
Ntabegera alinyongwa na watu hao kwa kutumia kitenge chake alichovaa.
Mwambalaswa
alisema Septemba 9 mwaka huu saa 8:00 mchana wakazi wa kijiji hicho,
walifanya msako wa kumtafuta Ntabegera baada ya kupotea Septemba 8 mwaka
huu.
“Baada
ya msako huo kufanyika, mwili wa marehemu ulikutwa kwenye kichaka
umbali wa mita 30 kutoka barabarani, ambapo mwili wake ulimwagiwa unga
kichwani na mgongoni,” alisema Kamanda.
Kamanda
alisema wauaji walitumia mfuko aliobebea unga Ntabegera akitokea
kusaga, kumvisha miguuni kisha mwili wake waliulaza kifudifudi. Polisi
inawasaka wahusika.
Post a Comment