Nyuma
ya tukio la denti wa darasa la tano kwenye shule moja ya msingi iliyopo
Mbezi-Shamba, Dar, aliyejitambulisha kwa jina moja la Irene (11) la
kunaswa akifanya utapeli kwa kuwaibia raia, mazito yameibuka.Katika
tukio hilo lililojiri hivi karibuni maeneo ya Posta Mpya, Dar, denti
huyo alikuwa akisimama nyakati za asubuhi akivalia sare za
shule huku akiombaomba kwa madai kuwa hana nauli ya kuvukia katika
kivuko cha Kigamboni kwenda shule anayosoma.
Kwa mujibu wa mmoja wa
mashuhuda, mtoto huyo alikuwa akisimama mbele ya Kituo cha Daladala
cha Posta mpya akijifanya ombaomba kwa madai kwamba hana nauli.Ilisemekana
kwamba siku nyingine mtoto huyo alikuwa akionekana akiuza simu kwa bei
chee na alipohojiwa alikokuwa akizitoa alidai ameziokota.
Mwandishi Gabriel Ng'osha (kushoto) akipata undani wa habari katika tukio hilo.
Dereva
mmoja, Juma Hamis anayeegesha gari lake eneo hilo (Posta Mpya) alisema
kuwa tabia ya mtoto huyo ilikuwa ni ya muda mrefu kwani alianzia
Kariakoo, Dar akitapeli na kuiba madukani ambapo watu walimstukia hivyo
akaamua kuhamia Posta.
“Mara kadhaa
amenusurika kupigwa akidaiwa kuchomoa simu za watu kwenye mikoba ndani
ya daladala.“Kukamatwa kwa Irene, watu wa maofisini na kwenye daladala
wameshukuru kwani anafahamika na ni tishio kwa utapeli na ndiyo
waliomchoma kwa polisi akadakwa baada ya kukutwa akijidai ni ombaomba,” alisema dereva huyo.
Ofisa wa Polisi kutoka 'Central Police' Posta akifafanua jambo kuhusiana na mkasa huo.
Jader
Sapi, anayefanya kazi katika ofisi moja zilizo ndani ya jengo la IPS,
alisema mtoto huyo aliwahi kuingia ofisini kwao na alipotoka,
wafanyakazi wawili walilalamika kupotea kwa simu zao, kitu
kilichowafanya wajue ni yeye.
Mama mmoja aliyeshuhudia Irene akichukuliwa na askari, alisema ameshawahi kumpa fedha mara kadhaa denti huyo, akiamini alivyomweleza kuwa hakuna na wazazi na hivyo hana nauli ya kumpeleka shuleni.
Akizungumza na gazeti
hili akiwa mikononi mwa polisi kwenye Kituo Kikuu, Irene alisema ni
mwanafunzi wa shule moja ya msingi (jina kapuni) iliyopo Mbezi-Shamba na
siyo kama alivyokuwa akidanganya kuwa anasoma Kigamboni, Dar.
Wananchi wakishuhudia laivu tukio hilo lililotokea maeneo ya Posta mpya, Dar es Salaam.
Pia
alikiri kwamba amekuwa akidanganya kuwa hana wazazi wakati ukweli ni
kwamba wazazi wake wapo.“Ni shetani tu aliniingia nikawadanganya raia,’’
alisema Irene.
Baada ya kushuhudia tukio hilo, wanahabari wetu walimsaka mkuu wa shule anayosoma mtoto huyo, Yusuph Zenny ambaye alikiri kumfahamu Irene na kudai kuwa tayari taarifa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi, Dar zilimfikia.
Alitobosa siri kuwa
ameshapata malalamiko mara kadhaa kuhusiana na binti huyo na kwamba
amekuwa akifanya uchunguzi ili kupata ukweli.
Hata hivyo, alisema
anawasiliana na wazazi ili kulifuatilia sakata hilo hivyo kuwaomba
wanahabari wetu wampe muda atatoa majibu au hatua itakayochukuliwahuku Irene akiwa bado mikononi mwa polisi kwenye dawati la jinsia.
Post a Comment