Mamlaka
ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imesema usajili
wa pikipiki maarufu kama ‘bodaboda’ utafanywa pamoja na kukagua namba
zenye rangi ya njano huku zikiwa zinafanya biashara, jambo ambalo ni
kinyume.
Meneja
Mawasiliano wa Sumatra, David Mziray alisema hayo Dar es Salaam wakati
akizungumza na mwandishi wetu kuhusu usajili wa namba za pikipiki
pamoja na zenye magurudumu matatu ili ufanywe pamoja na kukagua rangi
zinazotakiwa kwa biashara.
Usajili
wa namba za pikipiki na zenye magurudumu matatu unatarajiwa kufanywa na
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ambapo namba zote zitabadilishwa kuanzia
Oktoba mosi.
Akizungumzia
usajili huo, Mziray alisema kimsingi kazi hiyo itafanywa na TRA lakini
Mamlaka hiyo inaiomba Mamlaka ya Mapato kuendesha usajili pamoja na
ukaguzi wa rangi za namba za pikipiki.
“Zipo
bodaboda nyingi ambazo zina rangi za njano na ambazo zinaendelea kutoa
huduma kibiashara wakati rangi inayotakiwa ni nyeupe…tumewaambia TRA
wakati wa usajili huo wakague pia,” alisema Mziray.
Alisema
wamiliki wengi wa pikipiki wanapoagiza vifaa hivyo wakati wa kuvitoa
bandarini hudanganya kana kwamba sio vya biashara ili kukwepa kulipa
kodi lakini baadae huonekana mitaani vikifanya kazi kibiashara.
Alisema kutokana na usajili huo kufanywa na TRA, Mamlaka ya Sumatra itafanya ukaguzi huo ili kupunguza mianya ya wasiolipa kodi.
Kuhusu
usajili huo, taarifa ya Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi
ilifafanua kuwa TRA inawataka wamiliki wote wa vifaa hivyo kuwa mfumo
mpya wa usajili wa namba za pikipiki unaoanzia namba MC 101 AAA badala ya namba zinazotumika sasa.
“Kwa
mantiki hiyo wamiliki wote namba zote zitabadilishwa kuanzia Oktoba
mosi, hivyo wafike katika ofisi za TRA kwa ajili ya kazi hiyo,” alieleza taarifa hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, kazi ya ubadilishaji wa namba hizo utafanywa
bila adhabu kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Oktoba mosi mpaka Machi
31, mwakani na baada ya muda huo ubadilishwaji utafanywa na adhabu.
Post a Comment