Meneja Mkuu wa SSB, Sheikh Said Muhammad (kushoto) akikabidhi mfano
wa hundi ya Sh. milioni 10 kwa Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto (kulia).
Wanaoshuhudia ni viongozi wengine wa TASWA kutoka kushoto Shijja Richard
(Mweka Hazina), Amir Mhando (Katibu Mkuu) na Egbert Mkoko (Makamu
Mwenyekiti).
KAMPUNI ya Said Salim Bakhresa Group Limited, leo imetoa kiasi cha
Sh. Milioni 10 kwa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA) kwa ajili ya tuzo za Wanamichezo Bora nchini, zilizopangwa
kufanyika Desemba 12, mwaka huu.
Akikabidhi fedha hizo, Meneja Mkuu wa SSB Limited, Sheikh Said
Muhammad Said katika ukumbi wa City Sports Lounge, Mtaa wa Samora, Dar
es Salaam, amesema kwamba wanatoa mchango huo ili kuwezesha zoezi hilo
lifanikiwe.
“Kwanza nasema naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa niaba ya
kampuni kwa TASWA kutufuata kutuomba tuchangie tuzo hizi. Sisi tupo
mstari wa mbele katika kuunga mkono harakati zote za kimaendelea katika
sekta ya michezo nchini,”amesema.Sheikh Said amesema kwamba SSB
inajivunia kuwa sehemu ya shughuli hiyo na inawatakia kila la heri TASWA
ili wafanikishe mchakato huo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TASWA, Juma Abbas Pinto amesema kwamba
wanashukuru kwa mchango huo wa SSB, ambao unafungua mfuko wa fedha za
kuendehea zoezi hilo unaohitaji Sh. Milioni 120.
“Tumejiwekea utaratibu kwamba baada ya kufanya mazungumzo na watu
mbalimbali na kutukubalia kutusaidia zoezi hili, tutakuwa tunawatangaza
mmoja baada ya mwingine na kiwango wanachotoa,”.
“Kwa leo tunaanza na SSB, lakini tutarajie kama si Jumapili basi
Jumatatu tutakutana tena hapa hapa kwa ajili ya kumtangaza mdhamini
mwingine,” amesema Pinto.
Katibu wa TASWA, Amir Mhando kwa upande wake amesema maandalizi
yanaendelea vizuri na ameomba ushirikiano wa kutosha baina ya Waandishi
wa Habari nchini, ili zoezi hilo lifane.
Tuzo za wanamichezo Bora nchini, mwaka jana zilishindwa kufanyika
baada ya waliokuwa wadhamini wake, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)
kujitoa dakika za mwishon
Post a Comment