Dotto
Ndanga mwenye miaka 31 mkazi wa eneo la Mkwawa Manispaa ya Iringa
Mkoani Iringa amefariki baada ya kugongana na dereva mwenzake akiwa
anaendesha pikipiki yenye namba za usajili T:349 CCW aina ya SKYMARK
RACER.
Aidha
amesema marehemu amefariki wakati akitokea chuo kikuu cha Mkwawa
kuelekea maeneo ya Iringa mjini ambapo alikuwa akijaribu kuipita
pikipiki nyingine iliyokuwa mbele yake iliyokuwa ikiendeshwa na Joyce
Kiwale ambaye amekimbia baada ya kuitokea kwa tukio hilo chanzo kikiwa
ni mwendo kasi wa marehemu.
Hata
hivyo kamanda Mungi amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta
dereva aliyekimbia baada ya kutokea tukio hilo kwa uchunguzi zaidi pia
anatoa wito kwa wamiliki na madereva wa vyombo vya usafiri kuwa makini
wawapo barabarani kwa kuzingatioa sheria za usalama barabarani ili
kupunguiza ajali zinazoweza kuepukiaka.
Post a Comment