WATU
WANNE WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA GARI LENYE NAMBA
ZA USAJILI T.200 AKQ AINA YA ISUZU LORI IKIENDESHWA NA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA KUACHA NJIA NA KISHA KUIGONGA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA
USAJILI T.614 BUK AINA YA T-BETTER ILIYOKUWA PEMBENI YA BARABARA NA
KISHA KUPINDUKA.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 22.09.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO
MLIMA NYIMBILI, KATA NA TARAFA YA KAMSAMBA, BARABARA YA KAMSAMBA/MLOWO,
WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
WALIOFARIKI
KATIKA AJALI HIYO NI 1. SELA MKISI (30) MKAZI WA NTUNGWA 2. ENEA MGALA
(42) MKAZI WA NKANGA 3. LUSIANO MTENDA (50) MKAZI WA MKOMBA NA 4. ELITA
MASHAKA (02) MKAZI WA NTUNGWA.
AIDHA
WATU KADHAA WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA
MBOZI VWAWA KWA MATIBABU. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA
HOPSPITALI YA KAMSAMBA WILAYA YA MOMBA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA.
DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
Post a Comment