Mwanadafada ambaye ni mwanamitindo Bongo, Hamisa Mabeto ameamua
kumwanika mwandani wake baada ya kumuweka kwenye mitandao ya kijamii
huku akimmwagia sifa kemkem.
Akipiga
stori na mwandishi baada ya kuvutiwa waya,
Hamisa alisema mwanaume huyo ambaye ni miongoni mwa wakurugenzi wa redio
EFM aitwaye Dj Majay ni mtu ambaye anampenda sana na wana
malengo ya kuoana muda wowote kuanzia sasa na jina lake ataliweka
hadharani soon!
“Ni kweli ni mpenzi wangu ambaye tunapendana sana na muda wowote kuanzia sasa tutafunga pingu za maisha kama mipango yetu ikikaa vizuri,” alisema Hamisa.
Aliendelea kusema kuwa wana miezi sita mpaka sasa na amekuwa mtu ambaye anajua nini thamani ya mapenzi kwani muda wowote akimuhitaji anakuwa karibu yake.

Post a Comment