Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya kufua umeme ya Pan African Power Solution inayoimiliki kampuni ya
Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imezidi kung’aa katika nchi za
jumuia ya Afrika Mashariki katika kusambaza nishati ya umeme.
Hatua
hiyo inasababishwa na serikali ya Kenya kuipatia barua kampuni hiyo ya
kufanya nao kazi ya usambazaji umeme katika mradi unaohusisha nchi mbili
za jumuia hiyo, ambazo ni Tanzania na Kenya.
Barua
ya Kenya iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Petroli,
Injinia Joseph .K. Njoroge ya tarehe 19, Agosti 2014 kwenda kwa
Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, Harbinder Sing Sethi.
Taarifa
zaidi kuhusiana na barua hiyo, yenye kumbukumbu
nambaME&D/CONF/3/2/73A iliyokuwa na kichwa cha habari Expression of
interest for IPP for 2000MV power generations and supply to Kenya and
Tanzania.
Barua
hiyo, ilieleza kuwa inazitaka pande tatu hizo ikiwemo PAP, Tanzania na
Kenya kukutana haraka kuona ni namna gani uzalishaji huo utaanza haraka
iwezekanavyo.
Akithibitisha
barua hiyo, Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/PAP, Joseph Makandege
alisema kampuni yao inaendelea kuchapa kazi na haitishiki na kauli za
wanasiasa kwa kuwa wao si wanasiasa.
‘’Tunafurahi
kuwa tunazidi kuaminiwa na serikali mbalimbali ndani na nje ya
Tanzania. Hii inadhirisha ufanisi na ueledi wetu katika tasnia nzima ya
nishati,’’alisema.
Hivyo,
alisema anaamini maneno yote yanayoenezwa juu yao kuwa yanatawaliwa na
chuki na wivu wa kibiashara kutoka kampuni zingine za usambazaji wa
umeme.
Kutolewa
kwa barua hiyo kwa IPTL kutaweza kuondoa sintofahamu iliokuwepo, baada
ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR- Mageuzi) kudai kuwa
Seth anayeongoza kampuni hiyo amepigwa marufuku kufanya biashara ya aina
yoyote Kenya.
Kafulila
alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini hapa, kuwa Seth ni
fisadi na kwamba Kamati ya Bunge ya nchini Kenya imempiga marufuku
kufanya biashara nchini humo.
Post a Comment