Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakisalimiana na Askofu
Damian Kyaruzi wa Jimbo la Sumbawanga (kulia) katika Ibada ya kumweka
wakfu Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo
iliyofanyika kwenye kanisa kuu la kiinjili la Kilutheri la mjini
Sumbawanga Septemba 21, 2014. Wapili kushoto ni Mkuu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakimkabidhi zawadi
Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo (wapili kushoto)
katika ibada ya kumweka wakfu Askofu huyo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu
la Kiinjili la Kilutheri mjini Sumbawanga, Septemba 21, 2014. Kulia ni
mke wa Askofu huyo, Tunsume Mwaipopo na kushoto ni Askofu Israel
Mwakyolile wa Dayosisi ya Konde.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika ibada ya kumweka wakfu Askofu wa
Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo katika Kanisa kuu la
Kiinjili la Kilutheri mjini Sumbawanga Septemba 11, 2014.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kushoto) wakiwa katika Picha ya
pamoja na Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo na
mkewe Tunsume Mwaipopo (kulia) katika katika ibada ya kumsimika Askofu
huyo iliyofanyika kwenye Kanisa kuu la Kiinjili la Kilutheri mjini
Sumbawanga Septemba 11, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Post a Comment