Meneja
wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) Emmanuel Manderabona akiwaonesha waandishi wa habari mfumo wa
usambazaji umeme kwenye Moja kituo cha Mradi “Tanzania Energy
Development and Access Program (TEDAP)” unaofadhiliwa na Benki ya Dunia,
kilichopo Mbagala kitakachozalisha megawatt 100 za umeme, kituo hiki
kinatarajiwa kuanza kutoa huduma za umeme wa uhakika kwa wakazi wa
maeneo ya Kurasini, Kigamboni, Mbagala na Maeneo ya Mkuranga kuanzia
Mwezi Agosti, 2015.
Meneja
wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) Emmanuel Manderabona akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo
pichani) moja ya Transfoma iliyopo katika eneo la Mradi Mbagala lenye
MVA (MEGAVOLT-AMPERE) 50. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba.
Baadhi ya mafundi wakiedelea na kazi ya kusuka Transfoma iliyopo katika eneo la Mradi Mbagala lenye MVA (MEGAVOLT-AMPERE) 50.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba
akiwaeleza waandishi wa Mikakati inayowekwa na shirika hilo ikiwemo
kutekeleza miradi mbalimbali ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza
Umeme ili kuhakikisha wanakabiliana na Tatizo la Umeme Nchini,wakati wa
Ziara kwenye Mradi wa “Tanzania Energy Development and Access Program
(TEDAP)” unaotekelezwa katika maeneo ya Mbagala, Gongo la Mboto na
Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwaeleza waandishi wa
habari kufurahishwa kwake na ziara hii iliyoratibiwa Wizara ya Habari,
Vijana , Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na Shirika la umeme
Tanzania (TANESCO) yenye lengo la kuona nini Shirika hilo linatekeleza
katika jitihada za kukabiliana na Tatizo la Umeme Nchini.Kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi
Felchesmi Mramba.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akimweleza jambo
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi
Felchesmi Mramba (kushoto) wakati wa ziara kwenye Miradi ya umeme
Katika Eneo la Mbagala, Gongo la Mboto na Kinyerezi Jijini Dar es
Salaam.
Afisa
Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bi. Neema Mbuja
akiwaeleza jambo wahandisi Emmanuel Manderabona(Kushoto kwake) na Saimon
Jilima, wakati wa ziara kwenye Miradi ya umeme Katika Eneo la Mbagala,
Gongo la Mboto na Kinyerezi Jijini Dar es Salaam.
Meneja
wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) Emmanuel Manderabona akiwaonesha waandishi wa habari mtambo wa
kuongoza umeme uliopo katika eneo la Gongo la Mboto uliowekwa mfumo wa
Sakiti Mzunguko (Ring Circuit) kwenda Mbagala, Sakiti Mzunguko ni
Mzunguko mkubwa utakaotoa fursa ya upatikanaji wa umeme kwa muda wote
kwani umeme ukikosekana eneo moja ni rahisi kuunganisha kwa kupitia
upande wa pili na umeme ukaendelea kupatikana.
Mitambo
Miwili iliyofungwa katika kituo cha KINYEREZI ONE yenye uwezo wa
kuzalisha Megawatt 150 za umeme utakaogawanywa katika sehemu mbili
kuingia katika gridi ya Taifa, ikiwa ni kujenga msongo wa kilovolt 220
kwenda Kimara na kujenga laini ya msongo wa kilovolt 132 kwenda Gongo la
Mboto, Kituo hiki kitagharimu Dola za Kimarekani Milioni 183.
(PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO)
Post a Comment