Kesi
ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha imepigwa kalenda kwa
mara nyingine tena kwa sababu Hakimu anayeendesha kesi hiyo kupata
shughuli nyingine nje ya ofisi.
Mbasha alipanda kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya
Ilala kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yake hiyo ambapo mwendesha
mashtaka Kiyoja Catherine aliahirisha kesi hiyo kutokana na Hakimu
Williberforce Luwhego kupata dharura.
Kesi
hiyo imepangwa kusikilizwa tena 17 October mwaka huu ambapo Mahakama
itaanza kusikiliza ushahidi ambapo upande wa mashtaka utakuwa na
mashahidi wanne kwenye kesi hii inayomkabili mume wa Flora Mbasha
anaekabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo ya ubakaji.
Mara ya mwisho kabla ya hii kuahirishwa Flora Mbasha
alikwenda Mahakamani kwa mara ya kwanza akiwa na watu wake na hakukutana
wala kuongea na mume wake ambapo muda mfupi kesi hiyo ikaahirishwa.
Post a Comment