Jeshi la polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga Jana lililazimika kutumia risasi za moto baada ya wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuua watuhumiwa kisha kuwachoma moto.
Inasemekana watuhumiwa hao walivamia chumba ya mkazi mmoja wa mtaa wa Muhungula Kahama na kujeruhi kwa mapanga watoto wawili usiku wa kuamkia jana.
Kwa mujibu wa habari kutoka wilayani Kahama, juzi usiku watu 7 wanaodaiwa kuwa ni vibaka walivamia nyumba ya mtu kisha kujeruhi watoto wawili.
Kufuatia tukio hilo wananchi walianza kufanya msako kubaini watuhumiwa hao ,ndipo wakakamata wawili kati yao na kuanza kuwachoma moto.
Kufuatia tukio hilo wananchi walianza kufanya msako kubaini watuhumiwa hao ,ndipo wakakamata wawili kati yao na kuanza kuwachoma moto.
Wakati tayari wananchi wameshaua mmoja,jeshi la polisi lilifika kwa ajili ya kumwokoa mmoja,lakini wananchi hawakukubaliana na hali hiyo wakaanza kushambulia kwa mawe gari la polisi ndipo jeshi la polisi likaanza kufyatua risasi za moto.
Maafisa wa jeshi la Polisi wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wakiwa katika eneo la tukio kwa ajili ya kuuchukua mwili wa Marehemu.
Post a Comment