Mwalimu wa Shule ya Msingi Makurumla, Maria Samuel Hoza akiwa katika harakati za kufunga ndoa yake ya pili.
MWALIMU mmoja wa Shule ya Msingi Makurumla iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam, Maria Samuel Hoza, amejikuta akiaibika vibaya baada ya mumewe, Bryton Muhanje kumkuta akiwa katika hatua za mwisho za kufunga ndoa nyingine kwenye Kanisa Katoliki la Kigogo Luhanga, Jumamosi iliyopita.
Gazeti hili lilimshuhudia Muhanje, akiingia kanisani na kwenda moja kwa moja mbele ya altare na kumzuia Padri Richard, ambaye alikuwa amemaliza kufungisha ndoa ya kwanza, asifanye hivyo kwa maharusi wanaofuata kwa vile ni batili.
Chanzo chetu makini cha habari kililidokeza
gazeti hili juu ya kuwepo kwa mpango wa mwanamke ambaye yupo katika
ndoa, kutaka kuolewa tena na mtu mwingine bila mumewe kujua. Kufuatia
‘tip’ hiyo, kikosi kabambe cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM)
kilifanikiwa kupata namba ya mwanaume huyo na kufanya naye mawasiliano
ili kujua ukweli wa madai hayo.
Pamoja na hivyo, mwanaume huyo pia
alikwenda hadi shule anayofundisha mwalimu huyo na kwa kuwa hawamfahamu,
alijitambulisha kama ndugu yake na kwamba alikuwa anaomba kujua kanisa
ambalo (mkewe) atafunga ndoa, kwani ameelezwa kuwa lipo Magomeni lakini
hakuelewa ni lipi.
“Wanafunzi wa pale wakaniambia siyo Magomeni, bali ndoa inafanyika Kigogo Luhanga, ndipo nilipowasiliana na wenzangu na kuwaeleza habari hiyo, nikaongozana na baadhi ya wanafunzi ambao pia walikuwa wanakwenda kwenye harusi hiyo,” alisema.
“Wanafunzi wa pale wakaniambia siyo Magomeni, bali ndoa inafanyika Kigogo Luhanga, ndipo nilipowasiliana na wenzangu na kuwaeleza habari hiyo, nikaongozana na baadhi ya wanafunzi ambao pia walikuwa wanakwenda kwenye harusi hiyo,” alisema.
Ratiba ilionyesha kwamba ndoa ya wawili hao ilikuwa ya pili, hivyo mara tu zamu yao ilipofika na Padri Richard kuanza kutoa risala ya kuwapongeza kwa hatua waliyofikia, wote walionekana kuwa na bashasha ya siku hiyo muhimu ya kuungana.
Ghafla bila kutarajia, wakati wasaidizi wa
padri wakimletea kibakuli chenye pete ya ndoa, Muhanje alijitokeza na
kumuomba mchunga kondoo huyo kusitisha zoezi hilo kwa vile anayetaka
kufunga ndoa, ni mke wake halali.
Mume akiwa ameongozana na mpambe wake aliyesimamia ndoa yake, alimuomba padri atoe vielelezo kuthibitisha ukweli huo na baada ya kupewa nafasi hiyo, alionesha picha mbalimbali za siku ya harusi yao, nakala ya cheti cha ndoa na akaomba pia aruhusiwe atoe kompyuta yake mpakato ili achezeshe video ya siku hiyo ya Oktoba 29, 2009 alipofunga naye ndoa katika Kanisa la KKT Kimara Korogwe, Dar.
Kwa ushahidi huo, padri huyo alikubaliana
naye na kusimamisha zoezi hilo na kuwataka kuongozana kwenda ofisini kwa
mazungumzo zaidi. Baada ya mazungumzo marefu ofisini, padri huyo
alikubaliana na hoja za mume na hivyo kusitisha zoezi hilo, akidai
mwanamke huyo hawezi kuolewa kwa mara ya pili.
Ilifahamika baadaye kuwa Maria, ambaye amezaa mtoto mmoja na Muhanje, alitumia jina la Neema Stanley Hoza katika kusudio lake la kufunga ndoa ya pili.
Baada ya tukio hilo, Muhanje alisema
alimuoa mkewe mwaka huo, baada ya kuwa ameishi naye kinyumba kuanzia
mwaka 2005.“Baada ya kukaa naye kwa miaka minne, tukaamua kufunga ndoa
mwaka huo wa 2009 na baada ya hapo, yeye akaenda kufanya kazi ya ualimu
Lushoto katika Shule ya Shambalai.
“Alifanya vituko vingi sana, wakati mwingine alifunga mlango na kuondoka na funguo na kwenda kwa dada yake na kulala huko huko, wakati mwingine aliamua tu kuvunja vitu bila kujali hadi mwaka jana mwezi wa nne alipoondoka moja kwa moja kwenda kusikojulikana.“Siku chache zilizopita ndipo nilipopata habari kwamba ana mpango wa kuolewa, ndipo nikaanza kufuatilia ili nijue.
“Nilipokuwa pale kanisani wakati wa kuzuia ndoa, yule mwanaume aliyetaka kumuona mke wangu, alinitishia kuwa atanikomesha, nimeenda polisi kuripoti maana siwezi kujua atafanya nini na nimefungua jalada lenye namba MAG/RB/8452/2014 KUTISHIWA KUUA KWA MANENO.”
CHANZO:GAZETI LA UWAZI
Post a Comment