Ile
ahadi ya Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli ya kununua kivuko kipya
kitakachotoa huduma ya usafiri kati ya Jiji la Dar es Salaam na mwambao
wa Bahari ya Hindi hadi Bagamoyo imetimia.
Taarifa
za uhakikia tulizozipata hivi punde ni kuwa kivuko hicho (Mv Dar es
Salaam) kilichokuwa kinajengwa huko Denmark leo kimeshuka majini na
tayari kuanza safari ya kuja Dar es Salaam ambapo kinatarajiwa
kufika/kutua Dar es Salaam kati ya wiki tatu mpaka nne zijazo.
Kivuko
cha MV Dar es Salaam kitakuwa na kasi kuliko kivuko chochote Afrika ya
Mashariki na hasa mwambao wa bahari ya Hindi ukiacha Afrika ya Kusini.
Kivuko
hiki ni muendelezo wa juhudi za Wizara ya Ujenzi za kupunguza
msongamano katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kujenga
barabara za New Bagamoyo (Kawawa JCT - Tegeta); ujenzi wa miundombinu ya
mabasi yaendayo haraka (Bus Rapid Transit Infrastructure - BRT) ikiwemo
kuanza ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka awamu ya pili ;
ujenzi wa ‘Flyover’ ya TAZARA na UBUNGO ; barabara za pete (DSM Outer
Ring Roads); barabara ya Dar es Salaam – Chalinze Expressway; kupanua
barabara ya lami sehemu ya Gerezani (KAMATA – Bendera Tatu) kutoka njia
mbili za sasa hadi njia nne; kujenga daraja la Kigamboni linalounganisha
Kurasini na Kigamboni, daraja hili linatarajiwa kukamilika mwakani
mwezi wa sita.
PICHANI
CHINI: Taswira mbalimbali zikionyesha Kivuko cha MV.Dar es Salaam
kikiwa kimeshushwa majini leo tayari kwa kuanza safari ya kuja Tanzania
kutokea nchini Denmark.
Post a Comment