Baada ya kuitandika Basle 5-0 katika Champions League, kisha wakaja
kuifumua Deportivo La Coruna 8 kwenye La Liga wikiendi iliyopita, jana
kipigo cha Madrid kilihamia kwa timu ya Elche katika La Liga.
Wakicheza kwenye dimba lao la Santiago Bernabeu Madrid walianza kwa
kuanza kufungwa goli na Elche kupitia mchezaji Gallego, lakini dakika
chache baadae Gareth Bale akasawazishia Madrid.
Cristiano akafungua akaunti yake ya magoli jana kwa kufunga penati
katika dakika ya 28, dakika baadae akaongeza kwa kichwa, kisha akafunga
la penati tena dakika 80 kabla ya kumalizia shughuli kwa la tano dakika
ya tisini ya mchezo.
Ronaldo akaweka rekodi ya kufunga hat trick ya 25 tangu alipojiunga
na Real Madrid mwaka 2009 – huku akiisaidia Madrid kutimiza magoli 18 ya
kufunga katika mechi 3 zilizopita.
Timu zilipangwa kama ifuatavyo:</strong
Real Madrid: Navas, Marcelo, Carvajal, Varane, Ramos, Kroos, Rodríguez, Illarramendi, Bale, Isco, RonaldoSubs: Casillas, Coentrão, Benzema, Hernández, Arbeloa, Nacho, Modric
Booked: Carvajal, Marcelo
Scorers: Bale 20′, Ronaldo 28′, 32′, 80′, 90′
Elche: Yagüe, Gallego, Pelegrín, Lombán, Cisma, Romero, Corominas, Rodrigues, Mosquera, Morales, Cristian de Jesus
Booked: Gallego
Scorer: Gallego 15′
Subs: Suárez, Roco, Herrera, Martín, Fajr, Pasalic, Tyton
Ref: Carlos Clos Gómez
At: 65,000
Post a Comment