Serikali ya Tanzania imeidhinisha zaidi ya shilingi bilioni 290, kwa
ajili ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura ili liwe la
kidijitali, zoezi litakaloendeshwa na kusimamiwa na tume ya taifa ya
uchaguzi - NEC.
Mwenyekiti
wa NEC Jaji Mstaafu Damian Lubuva, amesema hayo leo jijini Dar es
Salaam na kufafanua kuwa kutolewa kwa fedha hizo kutaiwezesha tume hiyo
kuanza mara moja uboreshaji wa daftari hilo, zoezi lililochelewa kwa
zaidi ya mwezi mmoja kutokana na kutokwepo kwa fedha.
Kuidhinishwa kwa fedha hizo kumekuja licha ya wadau viiwemo vyama vya
siasa, kuhoji wapi tume ya uchaguzi itazipata fedha hizo, kutokana na
bajeti iliyotengwa na bunge kwa ajili ya utendaji wa ofisi hiyo kuwa ni
zaidi ya mara kumi ya kiwango kilichopangwa kutumika kwenye uboreshaji
daftari la wapiga kura.
Mmoja wa wadau waliolalamikia fedha hizo ni Mwenyekiti wa Chama cha
upinzani cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba ambaye amesema inashangaza
kuona serikali inapanga matumizi ya fedha ambayo hayajaidhinishwa na
bunge.
Aidha, Profesa Lipumba ameongeza kuwa hata teknolojia itakayotumiwa
kwenye daftari hilo ina mapungufu mengi kwani tofauti na inavyoelezwa
kuwa itafanya uhakiki na utambuzi wa wapiga kura kuwa rahisi, teknolojia
hiyo imeonyesha mapungufu makubwa kwenye nchi ilikotumika ikiwemo nchi
za Kenya na Malawi.
Post a Comment