Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) Imeanza rasmi zoezi la Usajili na
Utambuzi wa Watu Mkoa wa Morogoro pamoja na uchukuaji alama za vidole,
picha na saini ya kielektroniki kwa wananchi wa Wilaya ya Kilombero
ambao zoezi la Ujazaji fomu za maombi ya vitambulisho lilishafanyika.
Kuanza
kwa usajili na Utambuzi wa Watu mkoa wa Morogoro kumefuatia kukamilika
kwa zoezi kama hili mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara ambapo sambamba na
usajili unaoendelea sasa mkoani Morogoro zoezi la uchukuaji alama za
vidole picha na saini ya kielektroniki limekuwa likiendelea katika
baadhi ya Wilaya za mkoa wa Pwani.
Mkoani
Morogoro; katika eneo la Mikese kijiji cha Fulwe tumeshuhudia msururu
wa watu wakisubiri kusajiliwa huku wengine wakiwa katika harakati za
kuingizwa katika Rejesta ya Makazi inayomilikiwa na Mamlaka za Serikali
za Mitaa na Vijiji. Kwa utaratibu wa sasa ili uweze kusajiliwa lazima
kwanza kuwa unatambulika katika serikali yako ya Mtaa/Kijiji na kuwa
umeorodheshwa katika Rejesta ya Makazi ya Mtaa au Kijiji husika.
Leo
ikiwa ni siku ya kwanza ya kuanza kwa zoezi hilo litakalodumu kwa siku
saba mpaka Jumapili ya tarehe 29/09/2014 wananchi wengi wameonekana
kuhamasika na kujitokeza kwa wingi katika siku ya kwanza tofauti na
mazoea ya wengi kujitokeza siku za mwisho za zoezi.
Changamoto
kubwa bado imebaki wananchi wengi kukosa Viambata msingi vya
kuwatambulisha kama vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya elimu ya msingi au
sekondari n.k jambo ambalo limekuwa likisisitiziwa sana na NIDA katika
kurahisisha utambulisho wa mwombaji. (Picha na Rose Mdami- NIDA)
Post a Comment