HUKU wadau mbalimbali wa Habari wakiwa wanalaani Vikali kitendo cha
Jeshi la polisi kuwapiga wanahabari wakati wakiwa kazini,tukio hilo
lilitokea Mwishoni mwa wiki iliyopita Makao makuu ya Jeshi la polisi
nchini ambapo mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema
Freeman Mbowe alipofikishwa polisi,
Katika hali ya kushangaza Serikali imesema haina taarifa juu
ya kupigwa kwa mwandishi,bali imesema inafahamu tu wanachama wa chama
cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ndio waliokwenda makao makuu ya
Jeshi la Polisi,na hawafamu kwamba kunawanahabari waliopigwa,
Kauli hiyo ya Kushangaza imetolewa leo jijini Dar Es Salaam na
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo,Asah Mwambene wakati alipokuwa
anatembelea Mradi wa Maendeleo wa Shirika la tanesco uliopo Mbagala
Jijini Dar Es Salaam,licha ya kuzungumia masuala mbalimbali kuhusu
Tanesco kufikisha Miaka 50 ya kutuo huduma,
Ndipo Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi alipomuuliza
Mkurugenzi huyo kwamba yeye kiongozi wa Waandishi wa habari
anazungumziaje kitendo cha Jeshi la Polisi kuwapiga waandishi wa habari
walipokuwa kazini wiki iliyopita.
Ambapo Mwambeni ambaye vilevile pia ni Msemaji wa Serikali
alisema hana taarifa za kupigwa waandishi wa habari bali anacho fahamu
yeye ni wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema
walikwenda polisi.
“Serikali haina taarifa za kupigwa kwa waandishi Serikali
inachojua ni wanachama wa chama cha Chadema ndio walikwenda kwenye jeshi
la polisi na sio waandishi wa habari,na tunachojua sio waandishi wa
habari waliopigwa,nakuomba tuzungumeze vitu vingine ”Alijibu Mwambene.
Baada ya Mwambene kuzungumza kauli hiyo,alitoka pembeni
akawa anaongea na Mwandishi wa Gazeti la Habari leo ambaye naye ni
Miongoni mwa Waandishi wa Habari waliopigwa na jeshi la polisi katika
Tukio hilo huku akirekodiwa na mwandishi wa Mtando huu bila ya yeye
kujua kwamba mwandishi wa Mtandao huu anayafuatilia mazungumo hayo
alisikika akisema
“Ni mwandishi mmoja tu anayelalimika sana kwenye Vyombo vya
Habari,ni Yule Josephat isango wa gazeti la Tanzania daima Yule tunajua
kabisa ni mwanachama wa chadema kabisa maana aliwai kugombania Ubunge
kupitia chama hicho na tunachojua sisi na hata polisi waliokuwa
wakimpiga wanamjua Yule ni chadema ndio maana wakampiga unategemea
serikali tufanyaje “alihoji Mwambene.
Kauli hiyo ya Mwambene inatafsiriwa tofauti na wadau wa
Masuala ya Habari kwani kuzungumza huku kunazidisha maswali mengi
kutokana na Idara ya habari maelezo ndio inayowasimamia Waandishi pamoja
na Magazeti.
Kwa Upande wake Mwandishi ambaye anashutumiwa na Mwambene
Josephati Isango wa Gazeti la Tanzania Daima,wakati alipokuwa anafanyiwa
mahojianao maalum na Mwandishi wa Mtandao huu jana jijini dare s
Salaam,ambapo alisema kwa sasa anajipanga kwenda mahakamani kumburuza
mahakamani Cp Chagonja,Polisi watatu waliompiga pamoja na Waziri Mkuu
Mizengo Pinda.
Post a Comment