Kuna taarifa zimeendelea kusambazwa
kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na maelezo kuwa: " Serikali
kupitia Shirika la Elimu Tanzania, TPDC kwa ushirikiano na kampuni za oil and
gas, wanatarajia kuajiri vijana wapatao 500 katika sekta hii mpya Tanzania
kuanzia mwezi Januari na Machi 2015, hivyo wameandaa crush program itakayoanza
6 Oktoba 2014.
Walengwa ni vijana wenye elimu ya form 4 na form 6 ambao watasoma kwa miezi 6 na kupelekwa kwenye ajira moja kwa moja baada ya kuhitimu!..kwa wale wenye elimu kuanzia diploma watasoma kwa miezi 3, kozi ya oil and gas management!...Ada kwa kundi la kwanza ni tshs 1,150,000 na kundi la pili ni Tsh 550,000. Kwa yeyote mwenye kuhitaji fursa hii akachukue fomu Shirika la Elimu Tanzania, application form ni Tsh 20,000 na deadline ni tarehe 30 Septemba 2014".

TPDC
inapenda kuwaeleza Watanzania kuwa habari hizo si za kweli na kwamba TPDC haijafanya
makubaliano yoyote na Shirika la Elimu kuhusu suala hilo. TPDC inawaasa
Watanzania kuchukua tahadhari ya matangazo ya aina hiyo na inapotokea,
tafadhali wasiliana nasi kwa namba za simu zilizooneshwa hapo nchini.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO,
SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI
TANZANIA
BWM Pensions Towers, Tower A,
Junction of Azikiwe /Jamhuri Streets
P. O. Box 2774,
Tel:
+255 22 2200103/4
Dar-es-Salaam,
Tanzania
Post a Comment