Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Godfrey Mtei akipokea zawadi ya saa ya
ukutani kutoka kwa Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, juzi mjini hapa.
Picha ya pamoja baadhi ya waganga wakuu wa wilaya na mikoa wakiwa na Mgeni rasmi , Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia.
Waziri
wa Tamisemi, Hawa Ghasia akikambishi zawadi ya saa ya ukutani Mganga
Mkuu wa Serikali,Dk Donan Mmbando,saa hiyo iliyolewa na Taasisi ya Lab
Eguip Limited.
Baadhi
ya waganga wakuu wa wilaya na Mikoa ya Tanzania Bara wakisiliza hotuba
ya Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia ( hayupo pichani).
Dk Frida Mokiti ( kushoto) akibadilishana mawazo na mwezake wakati wa mapumziko
Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, akiwa na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Donan Mmbando , baada ya waziri kufungua mkutano.
Na John Nditi, Morogoro
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI),Hawa Ghasia, amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa , na
Halmashauri za wilaya nchini kuongeza zaidi kiwango cha kuchukua
tahadhari katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ukiwemo wa Ebola.
Waziri
Ghasia alitoa agizo hilo jana mjini hapa wakati wa hotuba yake ya
ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Waganga wakuu wa mikoa, Halmashauri za
wilaya na wakurugenzi wa Hospitali za rufaa kutoka mikoa yote ya
Tanzania bara.
Kwa
mujibu wa Waziri huyo kuwa, hapa nchini ugonjwa huo haujathibitika
kuingia na Serikali imechukua tahadhari zote kuhakikisha kuwa ugonjwa
huo hauingii nchini na endapo utathibikika kuingia uweze kudhibitiwa
kikamilifu.
Hata
hivyo alisema , mwaka huu kumekuwepo na matukio ya hapa nchini na nje
ya nchi yaliyotufanya tuongeze zaidi kiwango cha tahadhari , na tukio la
kwanza ni la mlipuko wa ugonjwa wa Dengue , ambao uliwapata wagonjwa
1,384 kote nchini, na kusababisha vifo vya watu wanne , sehemu kubwa ya
wagonjwa walikuwa ni wa Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Waziri huyo , tukio la pili ni la ugonjwa wa ebola ,ambao
kwanza ulianzia nchi za Afrika Magharibi, na kati ya Machi hadi Agosti
mwaka huu , watu 3,069 waliungua ugonjwa huo.
Hivyo hadi
kufikia Agosti 28, mwaka huu ,ugonjwa huo umeua watu 1,552 na hivi
karibuni umeingia nchi ya Congo DRC na kufikia mwishoni mwa mwezi
uliopita watu 24 wameripitiwa kuugua .
“
Ni matumaini yangu kuwa katika mkutano huu , suala la magonjwa ya
mlipuko kama haya yatajadilikwa kikamilifu ili kila mmoja wenu awe
katika tahadhari kubwa” alisisitiza Waziri Ghasia
Hata
hivyo , Waziri Ghasia alitumia fursa hiyo kutoa shukrani za Serikali ya
Tanzania kwa Watu wa Marekani kupitia Shirika lao la CDC na Shirika la
Afya Duniani kwa kutoa vifaa na vifaa tiba kwa ajili ya kuzuia
maambukizi ya ugonjwa huo wa ebola.
Mbali
na tahadhari ya magonjwa ya mlipuko, Waziri Ghasia alisema , katika
ziara zake sehemu mbalimbali hapa nchini ameshuhudia juhudi zinazofanywa
na wadau katika kuboresha upatikanaji na utoaji wa huduma za afya na
ustawi wa jamii.
Kwa
mujibu wa Waziri huyo kuwa juhudi hizo ni kujenga vituo vipya vya
huduma za afya , kukarabatiwa vituo ambavyo havipo katika hali
nzuri kuongeza watumishi na upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na
kuimalisha utaratibu wa kukusanya mapato katika vituo.
Pia
ulimalishaji wa utoaji wa huduma kwa makundi maalumu hususan , wanawake
wajawazito, watoto chini ya miaka mitano na wazee katika baadhi ya
maeneo husika.
Hata
hivyo alisema ,kutokana na juhudi hizo, malalamiko kuhusu uhaba wa dawa
na vitendo vya rushwa yamepungua katika maeneo ambako juhudi hizo
zimekwishafanyika.
“
Nimefurahishwa na kasi ya ujenzi mpya wa Zahanati na Vituo vya Afya
.... juhudi hizi zinapaswa kupongezwa kwa vile ni utekeleaji wa Mpango
wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)” alisema Waziri Ghasia .
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Serikali , Dk Donan Mmbando, kabla ya
kumkaribisha waziri , alisema lengo la mkutano huo ni kujadili masuala
muhimu yanayolenga kuboresha huduma za afya na ustawi wa jamii hapa
nchini na pia kuainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi
wa wizara hiyo.
Hata
hivyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wataalamu hao wa sekta ya afya
kujipanga kukabiliana magonjwa ya mlipuko ukiwemo wa ebola na kutenga
maeneo maalumu kwa ajili ya kutolea huduma endapo kutakuwa na
udhibitisho wa dalili za wagonjwa katika maeneo yao.
Pamoja
na kuzungumzia changamoto zilizopo ikiwemo ya ya usimamizi wa utendaji
bora na uboreshaji wa mazingira ya kazi na y a watumishi , pia
aliwataka wataalamu wao kuangalia namna ya kukabiliana na ongezeko la
magonjwa yasiyoambukizwa ukiwemo wa saratani.
Kwa
mujibu wa Manga Mkuu wa Serikali, kuwa vituo vingi vya Afya vilijengwa
kwa kuangalia upande mmoja wa kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza na
kusahau mengine yasiyoambukizwa na kwamba hatua zaidi zinapaswa
kuchukuliwa ili kukabiliana nayo na kutaka yaingizwe kwenye mpango kazi
wa mwaka 2016.
Post a Comment