Warembo
15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014
wakisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam,
Tunda Man, wametoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la
kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara.
Pichani juu ni washindi wa tano waliofanikiwa kuingia fainali ya
shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini Dar es Salaam baada ya
wengine 15 kufanyika Arusha mjini. Na Father Kidevu Blog.
Warembo wenzao waliobakia wakishangilia burudani ya vipaji kutoka kwa washiriki wenzao.
wadau wa sanaa ya Urembo Babati wakifuatilia shindano hilo.
Mkuu
wa Wilaya ya Hanang, Christina Mndeme aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa
Manyara, akiwa na waratibu wa show hiyo, Mzee Ally Sumaye (kushoto) na
Mfanyabiashara Mohamad Bajwa.
Msanii wa Bongo Fleva Tunda Man akitoa burudani kwa wadau wa urembo Babati.
Ilikuwa ni shwangwe kwa warembo hao ambao wapo Mikoa yua Kaskazini kwa ziara ya kimafunzo katika hifadhi za Taifa.
Post a Comment