WATOTO sita, wakiwemo wawili wa kiume wenye umri wa miaka 8 hadi 14
wameharibiwa vibaya sehemu zao za siri baada ya kubakwa kanisani na watu
wanaodaiwa ni wachungaji.
Watoto sita waliobakwa kanisani na watu wanaodaiwa ni wachungaji.
Wakiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru walikopelekwa kwa
matibabu na kuangaliwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa, watoto hao
walidai kufanyiwa mchezo huo kwa nyakati tofauti na wachungaji watatu
wa kanisa hilo lililopo eneo la Feed Force, Kwamorombo jijini Arusha.
Mmoja wa watoto hao anayesoma darasa la 4 katika shule ya msingi
alieleza kuwa yeye na wenzake wamekuwa wakifanyiwa mchezo mchafu katika
kanisa hilo baada ya wachungaji hao kuwapatia shilingi 2,000 za kufungia
mdomo.
“Siku moja nilipofika shuleni wenzangu wakaniambia niende pale
kanisani tukapewe hela, nilipofika niliwaona wenzangu wengine
wakifanyiwa mchezo mchafu na mimi mchungaji aliniambia niiname
akanifanyia kitendo kibaya na kunipa shilingi 2,000, niliumia sana,’’
alisema mwanafunzi mmoja.
Mwanafunzi mwingine alisema amekuwa akitoroka shuleni na wenzake na
kwenda kwa watumishi hao ambapo huwaingiza katika kanisa hilo na
kujifanya wanawaombea baadaye huwafanyia mchezo mbaya.
Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema.
“Tukifika huwa wanatufungia ndani na kutuambia tuwanyonye, baadaye
wanatubaka na wakimaliza wanatuambia tukisema kwa mtu yeyote
watatuchinja na kutuzika ndani ya kanisa lao,” alisema denti
huyo.Wanafunzi hao walieleza kuwa watumishi hao huwarubuni kwa kuwaeleza
kuwa watawasaidia kuwasomesha iwapo watakuwa wakienda kwenye kanisa
hilo na kuwaingilia.
Mzazi mmoja wa watoto hao, Julius, mkazi wa Kwamorombo alisema mtoto
wake alimweleza kwamba amekuwa akifanyiwa mchezo mbaya na watumishi hao
baada ya kupewa shilingi 2,000.
Alisema aligundua hilo kufuatia tabia ya mtoto wake kuchelewa kurudi nyumbani.
Naye Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema
ambaye alifika hospitalini kuwajulia hali watoto hao alisikitishwa na
kitendo hicho na kulitaka jeshi la polisi lifanye uchunguzi wa kina kwa
kushirikiana na vipimo vya kidaktari ili kupata ukweli wa tukio hilo.
“Nimeongea na mkuu wa mkoa, Magesa Mulongo ambaye ameahidi
kulifuatilia kwa kina suala hili na kujua undani wake,’’ alisema Lema.
Kamanda wa Polisi Arusha, Leberatus Sabas. Hata hivyo, watoto hao
baadaye walihamishiwa katika Hospitali ya Seliani kwa ajili ya vipimo
zaidi huku taarifa za awali zikithibitishwa na daktari wa hospitali hiyo
kuwa, baadhi yao walikutwa na michubuko na kupanuka sehemu za siri hali
inayooneshwa kuingiliwa.
Watuhumiwa wa tukio hilo wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi
jijini hapa kwa uchunguzi zaidi na Kamanda wa Polisi Arusha, Leberatus
Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Post a Comment