Jeshi nchini Nigeria limesema zaidi ya wafuasi 260 wa Boko Haram wamejisalimisha Kaskazini mwa nchi hiyo. Jeshi
hilo limesema katika mapambano limemuua mtu mmoja ambaye huwa
anaonekana kwenye picha za video za propaganda za Boko haram akijidai
kuwa Kiongozi wa wa kundi hilo, Abubakar Shekau.
Jeshi
lilisema
kuwa wapiganaji 135 walijisalimisha wakiwa na silaha zao katika eneo la
Biu , jimbo la Borno siku ya Jumanne. Liliongeza kuwa wengine 133
walijisalimisha Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Hata hivyo mwandishi wa
BBC mjini Lagos Will Ross anasema kuwa ni vigumu kuthibitisha madai
hayo ya jeshi.
Mwaka jana jeshi lilisema kuwa Shekau huenda aliuawa , lakini halikutoa thibitisho lolote. Hata
hivyo ikiwa ni kweli kuwa wapiganaji hao wamejisalisha basi huenda ni
ushindi kwa jeshi la Nigeria katika vita vyake dhidi ya Boko Haram.
Mwandishi
wa BBC nchini Nigeria amesema kuwa majuma ya hivi karibuni Boko Haram
imeshindwa kwa kiasi kikubwa wakati walipokuwa wakipambana kudhibiti
eneo karibu na mji wa Maiduguri ambalo ni ngome yake.
Jeshi
limesema wafuasi 135 wa Boko Haram wamejisalimisha wakiwa na silaha zao
katika majimbo ya Biu na Borno,halikadhalika wafuasi wengine 133
wanahojiwa. Kwingineko , Rais wa Nigeria,Goodluck Jonathan amesema
kuwa zaidi ya watu 13,000 waliuawa katika miaka mitano ya kwanza ya
harakati za Boko Haram nchini humo.
Rais
Jonathan alisema hayo katika hotuba yake katika baraza la usalama la
Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya Jumatano. Rais Jonathan pia
alisisitiza kuwa juhudi zinafanywa kuwaokoa wasichana wa Chibok.Chanzo
BBC swahili
Post a Comment