Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen
Wasira
---
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen
Wasira amesema mgogoro wake na Jaji Joseph Warioba uliotokana na kura za
maoni ndani ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, ndiyo
uliomsukuma kujitoa chama tawala na kujiunga na NCCR-Mageuzi.
Hata hivyo, katika mahojiano maalumu na gazeti
hili, Wasira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda (CCM) amesema hajutii uamuzi
wake huo kwa kuwa anaamini historia imeandikwa.
Wasira aliingia kwenye mgogoro na Jaji Warioba
wakati mwanasheria huyo akiwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais
katika Serikali ya awamu ya pili na Wasira akiwa Waziri wa Kilimo.
Wasira alisema hakwenda NCCR-Mageuzi kwa lengo la
kufanya ushushushu na baadaye kurudi CCM kama alivyofanya mwaka 2000,
bali alikwenda huko baada ya haki yake kuminywa na viongozi wa CCM wa
wakati huo.
Alieleza kuwa baada ya uchakachuaji huo katika
kura za maoni, aliamua kwenda Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es
Salaam kukata rufaa, lakini hata huko hakutendewa haki, kwani rufaa
yake iliwekwa kiporo na ingesikilizwa baada ya uchaguzi mkuu.
Mgogoro ulivyoanza
“Nataka mwelewe kwamba mimi sikwenda upinzani kwa
sababu nilikuwa napingana na sera za CCM. Kwanza 1985 nilikuwa mbunge na
ndiyo maana Rais Ali Hassan Mwinyi aliniteua kuwa waziri wa kilimo,”
alisema Wasira na kuongeza;
“Mwaka 1990 niliacha kugombea kwa kumwachia Jaji
Warioba. Kwa sababu kama utakumbuka mwaka 1985 Warioba alikuwa
ameteuliwa kuwa mbunge na waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais.”
Wasira alisema aliamua kumwachia Jaji Warioba kwa
kumheshimu kwani aliamini ingekuwa kampeni ngumu kwamba waziri mkuu
anachuana na waziri wa kilimo, ingawa hata hivyo, alisema iwapo angeamua
kuchuana naye angemshinda.
“Lakini lile jimbo lilikuwa la kwangu kwa sababu
mimi ni kiongozi kutokea chini kwenda juu na mwenzangu Warioba ni
mwanasiasa wa kutokea juu kwenda chini,” alisema.
Wasira ambaye alionekana kuukumbuka vizuri mgogoro
huo alisema, “Hiyo ndiyo tofauti iliyopo. Kwa hiyo kama mimi ningeamua
kuchuana naye, angeshindwa mwaka huo wa 1990. Sasa faida yenyewe iko
wapi?” alihoji Wasira.
“Mimi nikaamua kujitoa si kwa kumwogopa Warioba,
hapana. Hii ilinipa sifa nzuri kwa sababu Mwalimu (Julius Nyerere)
aliniambia umefanya jambo la heshima sana,” alisema.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.......
Post a Comment