Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MBEYA City fc imepata pigo baada ya wachezaji wake watatu kuumia
katika mechi ya jumamosi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu iliyomalizika kwa
suluhu ya bila kufungana, uwanja wa Sokoine, Mbeya, na watakaa nje ya
uwanja kwa wiki mbili.
“Kwanza nianze na majeruhi; baada ya mechi kumalizika jumamosi
iliyopita, kuna wachezaji wetu watano walipata majeraha, lakini wawili
kati yao watarejea jumamosi ijayo kucheza dhidi ya Coastal Union
kwasababu maumivu yao hayakuwa makubwa sana. Wachezaji hao ni beki
Deogratius Julius ‘Musafwa wa Kweli’ na kiungo mahiri, Steven Mazanda.”
Alisema Dismas.
“Wachezaji wengine watatu kwa maana ya John Kabanda, Alex Seth na
Eric Mawala, hawataweza kucheza kabisa siku ya jumamosi kwasababu
watakaa nje kwa majuma mawili, kwa mujibu wa daktari wetu.”
Dismas aliongeza kuwa maandalizi ya mechi ya pili nyumbani yanakwenda
vizuri na wachezaji wana morali ya kutafuta ushindi na kuendeleza
rekodi yao ya msimu uliopita ambapo walimaliza katika nafasi ya tatu
nyuma ya Yanga na mabingwa Azam fc.
“Hali ya kambi ni nzuri, tunajiandaa vizuri na tunaamini tutaibuka na
ushindi. Tulicheza mpira mkubwa sana dhidi ya JKT Ruvu, sema wakati
mwingine demokrasia ya mpira wa miguu inabidi tukubaliane nayo”
“Kuna kushinda, kushindwa na kutoa sare, lakini mwisho wa siku
tulicheza mpira mzuri na watu waliokuwepo uwanjani waliridhika na
kiwango cha timu”
“Tunataka kulipa kisasi, Coastal walitufunga na kutuharibia rekodi
yetu. Tunataka kuonesha kwamba kutufunga kwao sio kwamba tulikuwa chini
ya kiwango bali walitubahatisha tu”
Post a Comment