Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Prof. Makame Mbarawa akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Utiaji Saini Mkataba
wa Utendaji baina yake na Wenyeviti wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya
Wizara kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi zao kwa mwaka wa
fedha wa 2014/2015.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote,Prof. John Nkoma akiweka saini
mkataba wa utendaji baina yake na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia,Mhe. Prof. Makame Mbarawa kwa ajili ya utekelezaji wa
majukumu ya Taasisi kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. Prof. Makame Mbarawa
akipeana mkono na Prof. Nkoma baada ya kuwekeana saini mkataba.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Prof. Makame Mbarawa ameongoza
zoezi la utiaji Saini Mkataba wa Utendaji baina yake na Wenyeviti wa
Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara kwa ajili ya utekelezaji wa
majukumu ya Taasisi zao kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.
Lengo
la Mhe. Waziri kuwekeana saini Mkataba wa Utendaji na Wenyeviti wa Bodi
ni kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa majukumu ya Wenyeviti wa Bodi
hizo ili kuleta ufanisi na tija kwenye Sekta ya TEHAMA, Sayansi na
Teknolojia ili iweze kuendelea kuchangia ukuaji wa uchumi na mchango wa
sekta kwenye pato la Taifa.
Aidha,
Mhe. Mbarawa alisema kuwa mapitio ya utekelezaji wa mkataba huo
utafanyika kila baada ya miezi mitatu ili kufuatilia namna
unavyotekelezwa na kubaini changamoto zinazowakabili wenyeviti wa Bodi
za Taasisi zilizo chini ya Wizara kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha wa
2014/2015.
Taasisi
zilizo chini ya Wizara ni pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Kampuni ya Simu Tanzania,
Shirika la Posta Tanzania, Taasisi ya Sayansi na Teknolojia, Chuo Kikuu
cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya
Nelson Mandela, Tume ya Nguvu za Atomii Tanzania na Mfuko wa Mawasiliano
kwa Wote.
Post a Comment