“MADAM...Madam...Madam...” ndizo kelele zilizosikika wakati Beutiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ alipokuwa akimtunza fedha nyingi dogo machachari wa Bendi ya Yamoto, Asilahi Isiyaka ‘Dogo Aslay’.
Aslay akimwagiwa minoti na Beutiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’.
Tukio hilo limetokea ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem
na kuweka historia kwa Wema kuwa staa wa kwanza ‘kumwaga’ fedha wakati
wa uzinduzi wa bendi ya Yamoto.
Awali, wakati bendi ya Yamoto ilipokuwa ikitumbuiza, ulifika wakati
kiongozi wa bendi hiyo, Said Fella alitambulisha uwepo wa Wema kwa kudai
amemuwakilisha
bebi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivyo apande jukwaani na kusema
chochote lakini mrembo huyo akasema kilichompeleka ukumbini hapo ni
uzinduzi wa Yamoto Band.
“Jamani nimekuja hapa kwenye uzinduzi wa Bendi ya Yamoto na siyo kumuwakilisha Diamond,
ya huku hayamuhusu kabisa sasa semeni niwaimbie wimbo gani,” alisikika
Wema Sepetu na kuanza kuimba wimbo wa Niseme ambao mashabiki
waliupendekeza.
Aslay akifurahiya minoti aliyomwagiwa na Beutiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’.AMWAGA FEDHA
Mrembo huyo asiyechuja tangu alipotwaa taji la u-miss Tanzania (2006), akiwa na wapambe wake, baada ya kuimba kidogo, alichukua pochi yake na kuanza kummwagia fedha mfululizo Dogo Aslay huku akiwa anamzunguka kwa kucheza.
ASLAY APAGAWA
Kwa fedha hizo zilizokadiriwa kuzidi milioni moja alizotunzwa Aslay, ilifika wakati dogo huyo akawa anaziangalia tu kama bubu na kupigwa butwaa hukuakiishia kuzitazama bila kuimba chochote. BAUNSA AMZUIA WEMA
Katika hali iliyowashangaza wengi, baunsa mmoja aliyekuwa akimlinda
Wema alimzuia staa huyo kuendelea kutoa fedha zaidi akidai zimetosha
ndipo akaacha na kushuka jukwaani.
Wema Sepetu ‘Madam’ akiwa na marafiki zake. KWA NINI ASLAY TU?
Wakati zoezi hilo likiendelea,
kuna baadhi ya mashabiki waliibua minong’ono wakihoji kwa nini atunzwe
Aslay peke yake wakati bendi hiyo ina wakali wengine watatu, Malomboso,
Enock na Beka?
“Mbona kama anampendelea Aslay tu wengine hawatunzi ona hela zote
ameshikilia yeye tu kweli, inaonekana anamzimia sana Aslay, si bure,
haikatazwi lakini,” alihoji shabiki mmoja aliyekuwa akifuatilia shoo
hiyo.
Wema ameonekana kuja juu kwa sasa kifedha, wiki iliyopita alifanya
tukio kama hilo katika Ukumbi wa Thai Village Masaki kwa kumtunza ‘pesa
ndefu’ mwanamuziki wa Bendi ya Skylight, Sam Mapenzi huku ikidaiwa
ni mwendelezo wa kampeni ya kumziba mdomo aliyekuwa shosti wake, Kajala
Masanja ambaye inadaiwa kwa sasa yuko ‘vizuri’ kifedha.
Post a Comment