Ajali
mbaya imetokea jioni ya leo katika eneo la Tengeru,Jijini Arusha
ikihusisha gari dogo aina ya Toyota Hiace (pichani juu) linalofanya
safari zake kati ya Usa River na Katikati ya mji wa Arusha na Lori la
Mafuta. Chanzo cha Ajali hiyo inaelezwa kwamba ni hiyo daladala lilikuwa
likijaribu kulipita gari jingine ndipo likakutana na loli hilo la
mafuta na kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya abiria wote
waliokuwa kwenye daladaa hilo ambao idadi yake haijafahamika
rasmi.taarifa kamili itawajia baadae kidogo.Picha na Dixon Busagaga wa
Globu ya JAMII Kanda ya Kaskazini.
Loading...
Post a Comment