Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii
Hatimaye
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemwachia kwa
dhamana Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya (bongo fleva), Rashidi
Makwaro (29), maarufa kama Chid Benz, baada ya kutimiza masharti ya
dhamana ya mahakaman hiyo.
Chid
Benz, alifikishwa mahakamani hapo jana akikabiliwa na mashitaka matatu
ikiwemo kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh.
38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na
kigae.
Hakimu
Mkazi Mkuu, Warialwande Lema alisema mshtakiwa alitakiwa kuwa na
wadhamini wa wawili wanaotoka kwenye taasisi zinazotambulika na wasio
walimu pamoja na kusaini hati ya dhamana ya Sh. milioni moja.
Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Inspekta Jackson Chidunda.
Wakili
Kombakono alidai kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika uwanja wa Ndege wa
Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa
dawa za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa gramu 0.85.
Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa alikutwa na gramu 1.72 za bangi isivyo halali.
Wakili
huyo wa serikali alidai kuwa, siku na eneo la tukio la kwanza na la
pili, mshtakiwa alikutwa akiwa na vifaa vinavyotumika kuvutia dawa za
kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku akijua ni kosa.
Mshtakiwa alikana mashitaka yote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Hakimu Lema alisema kesi hiyo itatajwa Novemba 11, mwaka huu.
Post a Comment