Stori: Mwandishi Wetu
HUKU mwenyewe
akikanusha vikali kwamba hatumii, nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose
Muhando bado anaandamwa na madai mazito kwamba anatumia madawa ya
kulevya ‘unga’ yanayomfanya kuwa hoi kiasi cha kushindwa kutokea kwenye
matamasha mbalimbali anayolipwa fedha, Risasi Jumatano linateremka nayo.
Kwa
mujibu wa vyanzo, Rose anadaiwa kutumia unga kiasi kwamba, baada ya
matumizi hujikuta akishindwa kufanya jambo lolote lile la kujitafutia
mkate wake wa kila siku na ndiyo maana amekuwa akikwaa skendo za kupokea
fedha za shoo halafu hatokei tu!
WATOA MADAI
Hivi
karibuni, akina mama watatu walifika kwenye Ofisi za Global Publisheers
na kumtolea madai Rose kuhusu tuhuma zanazomwandama kwamba amekuwa
akiingia mitini na fedha za watu wanaomwita kwenye matamasha ya nyimbo
za Injili.
“Sisi
tunavyojua, Rose anatumia madawa, wengine wanasema unga wengine
wanasema sijui nini huko. Sasa akishatumia hayo madawa huwa yanamfanya
awe kama amelewa na kushindwa kufanya lolote.
“Huwa
anafika hatua anashinda kitandani amelala tu na hawezi kutoka, ndiyo
maana mtu anaweza kumpa pesa asitokee kuimba kwa sababu anashindwa
kutoka ndani kwake.
“Kwa
hiyo jamani, si suala la kumwandika tu kwamba anaingia mitini na fedha
za watu bali mumsaidie Rose kama kweli mnampenda, sisi wenyewe
tunamwombea kwa Mungu kila siku,” alisema mama mmoja kati ya hao
waliofika lakini bila kutaja majina yao.
MADAI SUGU
Madai
ya kwamba, Rose anatumia madawa ni ya siku nyingi, wengi wamekuwa
wakisema wana uhakika, wengine wanasema wanasikiasikia tu lakini hawana
uhakika.
Magazeti
ya Global (Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi Jumatano, Amani, Ijumaa na
Risasi Jumamosi) yameshapokea madai hayo kwa muda mrefu lakini
kilichokuwa kikifanyika ni kuendelea kumchunguza msanii huyo kuhusu
madai hayo.
RISASI LAINGIA KAZINI KUCHUNGUZA
Kufuatia
madai ya akina mama hao waliojitambulisha ni waumini wa kutoka katika
kanisa moja la kilokole jijini Dar, gazeti hili liliamua kuingia kazini
kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli au uongo wa madai hayo.
WATU WA KARIBU NA ROSE
Mtu
wa kwanza kumtafuta ambaye gazeti hili liliamini kwamba anaweza kujua
chochote kuhusu madai hayo ni mratibu wa Tamasha la Pasaka linalofanyika
kila mwaka kwenye baadhi ya mikoa, Alex Msama.
Msama: “Mimi siwezi kusema ni kweli kwani sijawahi kumwona akitumia wala sijui kama ameathirika.”
Risasi Jumatano likamsaka
Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania (Chawaita), Stela Joel:
“Mimi sijui, kama unasema kuna watu wamekuja ofisini kwenu na kutoa
madai hayo, basi wamwombee. Lakini tutachunguza.”
MCHUNGAJI
Risasi
Jumatano pia lilibahatika kuzungumza na mchungaji mmoja (jina tunalo)
ambaye alisema ameshawahi kusikia taarifa hizo akamuuliza Rose lakini
alimkatalia kuwa si madai ya kweli.
“Ila
ninachojua mimi ni kwamba, Rose amekuwa akitumia dawa f’lani (akazitaja
jina). Hizi ni dawa zinazopatikana kwa njia ya sindano. Mara nyingi mtu
akiwa hajiwezi kwa maana ya kushindwa kufanya kazi anachomwa hizi
zinampa nguvu.
“Niliwahi
kusikia kwamba, kuna daktari mmoja katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma
(akamtaja jina). Huyu ndiye aliyekuwa akimchoma sindano zenye dawa hizo
Rose pale mwili unapokuwa dhaifu.
“Ila
madhara yake sasa, dawa ikiwa imekwisha mwilini, mtu anakuwa mlegevu,
anahisi kizunguzungu au kulalalala, kutokwa jasho jingi na kuhisi
anaumwa kiasi kwamba ukimwona unaweza kusema ni teja. Ni dawa ghali sana
kwa dozi moja, nadhani ni shilingi laki sita,” alisema mchungaji huyo.
Akaongeza:
“Nasikia Rose amefika mahali huwa anajichoma mwenyewe akipata dozi. Kwa
hiyo kwa suala la kubwia unga nadhani alilikanusha.”
ROSE MWENYEWE SASA
Risasi Jumatano, juzi
lilimpigia simu Rose lakini hakupokea hata baada ya kurudia kumpigia
mara kadhaa. Likamtumia meseji na kumsomea mashitaka yote, akajibu:
“Samahani
sana nawaomba mnipumzishe kuniandika...najua ni nani na kwa nini
ananitenda hivyo, ni kwa sababu anataka kunitumia kwa faida yake na ni
mtu hatari sana kwangu na kwa taifa zima.
“Mtu huyo anafanya haya ili kuniziba mdomo kwani najua siri zake nyingi na nzito, nashindwa kusema ataniua.”
Hata hivyo, Rose alipotakiwa kumtaja kwa jina mtu huyo ambaye Risasi Jumatano halimjui, alikataa katakata akisema anaogopa!
Post a Comment