Kwa
hali ya kushangaza, kituo cha television cha matangazo cha tbc 1 kati ya
vituo vinne maarufu vya matangazo ya habari nchini Tanzania kimeshika
nafasi ya mwisho baada ya kufanyiwa utafiti,
Kwa
habari za uhakika ni kwamba kituo kilichoongoza kuangaliwa na watazamaji
wengi ni ITV kikifuatiwa na Star TV, nafasi ya tatu imeshikwa na
Channel 10 na hatimaye TBC1.
Kwa
utafiti uliofanya na na TCRA imebainika kuwa ni aibu kama kituo
television ambacho ni cha Taifa na ni UMMA kushika mkia nyuma ya vituo
binafsi jambo ambalo ni hatari.
Vyanzo
vya kuaminika vinadai kuwa TBC1 imefikia hapi baada ya kugundulika
inabagua baadhi ya habari ya vyama vya siasa na kutoa habari ya chama
kimoja tuu jambo ambalo siyo sahihi katika utashi wa utangazaji na
kutofuata uhuru wa kiutangazaji ndani ya uongozi wa shirika la habari la
Tanzania,
Utafiti
umeonyesha kuwa ili chombo cha habri kiweze kuangaliwa na watu wote wa
vyama vyote ni lazima chombo cha habari kitoe habari bila kubagua vyama
vya siasa maana watazamaji wana misimamo tofauti na itikadi tofauti, na
kama chombo cha habari kikiamua kutoa habari kwa chama kimoja cha siasa
basi ujue hapo watakaoangali hizo taarifa za habari ni hao hao wa chama
kimoja.
Watafiti
pia walienda mbali zaidi na kukinyoshea vidole kituo cha taifa cha
utangazaji kuwa ni chombo cha UMMA na kisipende kubagua baadhi ya
taarifa za habari za vyama vya siasa kwa misingi ya kuelekezwa na
wanasiasa au viongozi wa nchi maana madhara yake ni wananchi kushindwa
kuangalia hicho kituo.
Mwisho
wake kitashindwa kufanya biashara na hatimaye kutegemea tuu ruzuku
serikalini na hapo ndo nchi itazidi kupata hasara badala ya kukiacha
chombo kijiendeshe kwa uhuru. Wametoa mfano kama shirika la habari la
Uingereza BBC lingefanya kama TBC inavyofanya basi nayo ingeishia
kutazamwa tuu nchini uingereza na tena kwa watu wachache tofauti na
ilivyo sasa BBC inatazamwa duniani kote.
Utafiti
umeonyesha kuwa hivi vyombo vingine vya habari ITV, Star TV na Channel
10 vimepata watazamaji wengi kwa kuwa havibagui matangazo ya kada
tofauti ya vyama vya siasa na hapo ndoo inasababisha waweze kupata
watazamaji wa kutosha.
Post a Comment