Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova,
amethibitisha kuwa Jeshi lake limefanikiwa kumkamata jambazi sugu
aitwaye Paulo Thamas Milanzi maarufu Chinga (35), Mmakonde mkazi wa
Chanika.
Amesema baada ya majibizano ya risasi jambazi hilo lilijeruhiwa na
kufikishwa hospitali ya Muhimbili kwa matibabu lakini baadaye alifariki
dunia.
Alisema jambazi huyo lilikuwa akitafutwa na polisi kutokana kuhusika kwenye matukio ya mauaji na wizi ikiwemo tukio la kuuawa kwa Afisa Mwandamizi wa Usalama wa Taifa, Sylivabus Adrian Mzeru Aprili 29, 2014 liliotokea Uwanja wa Ndege.
Aliongeza kuwa Chinga alikamatwa na bastola aina ya Star.'

Majambazi wenzake walikamatwa na kwa sasa wako gerezani wakisubiri taratibu za kisheria kuchukua mkondo wake.
Post a Comment