SIku za hivi karibuni kumekuwepo na kutoelewana kati ya
wanachama wanaounda kundi la Bongo Movies lililokua likiongozwa na
Steve Nyerere kabla hajajiuzuru huku chanzo kikiwa ni majungu kati ya
wanaounda kundi hilo. Majungu hayo ndo yamepelekea mpaka baadhi ya
wanachama wake kulikimbia.
Leo kupitia Instagram mwanadada Didas Facion katika ukurasa wake
amefunguka kuhusu mkasa uliomkuta hadi movie yake kukataliwa kuuzwa
Bongo. Mwanadada huyo mwenye makazi yake nchini Uingereza aliamua
kuchukua wasanii wa Bongo Movie na kuwapeleka kuigiza movie yake huko
Uingereza. Inadaiwa kua hapo mwanzo alichagua wasanii mbalimbali huku
mmoja wao akiwa ni Frank.
Kabla hajamaliza makubaliano na Frank Didas anasema kua alipokea simu huku aliyepiga simu hiyo akimwambia maneno ya uongo kumhusu Frank. Hiki ndo alichokiandika Dida ” Jamani mnamuona huyu kaka hapa? Huyu kaka anaitwa Frank kwa wale msio mjua. Huyu kaka ndio alikuwa aje UK kucheza movie ya MATESO YANGU UGHAIBUNI.
Na tulisha kubaliana hadi bei maskini na kila kitu kilikuwa poa. Mara ghafla nikapokea simu ya kinafki, na wakati huo mie nilikuwa sijui lolote kuhusu bongo movie. Nikaambiwa huyu kaka ninae taka kumchukua hajui kucheza wala ku direct movie. Nika pampiwa vibaya mnoo mpaka nikatia akili. Frank kokote ulipo naomba unisamehe najua ulikuwa tayari umekuwa na tamaa ya safari ya kuja ulaya, ila waziba rizki wakafanya yao. Wacha naishi hapo. Hii ni intro tu. Hadithi kamili inakuja. Kaeni na ndimu zenu.”
Baadae Dida aliamua kufunguka kuhusu movie yake hiyo kuzuiliwa kuuzwa Bongo huku akidai chanzo kikubwa ni msanii Clouds wa Bongo Movie. Hiki ndo alichokisema DIda kumhusu Clouds ” Haya uliniita mimi tapeli tena mzulumati, nimekudhulumu million 8 za kuja kucheza movie, ukaenda mpaka kwenye magazeti kusema, nikapigiwa na wenye magazeti, nikawapa ukweli na ushahidi. Tena huu ni mfano tu, ninazo nyingi na za aibu, na bado naendelea. Frank aliniomba nimlipe Tsh 2 million kucheza hiyo movie, nikakubali, wewe ukasema kila kitu utafanya bure ila nikisha uza movie nikufikirie, sasa leo umemfanya @stevenyerere2 kajiuzulu eti kisa kanisaidia uzinduzi, na hela ya PSPF tumekula, huu ni mfano nakuja kumwaga mengi. Ulijitole kila kitu bure uje ulaya, leo umenipaka mavi dunia nzima mimi tapeli, unawafanyia fitna watu wote wanao kaa karibu na mimi. Hii ni haki? Sawa mimi tapeli dhulumati, zote ni njia za kutafuta riziki. Tutafika hata mahakamani. Bado na rudi na mazito zaidi. Ongezeni ndimu. ”
Baada ya Dida kufunguka hivyo Batuli ambaye pia yupo Bongo Movie alimuomba DIda apunguze hasira na aache kuweka ukweli huo mtandaoni. Bado tunaendelea kufatilia ukweli wa jambo hili na soon tutakuja na jibu kamili.

Post a Comment