Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CCM: MAKUBALIANO YA RAIS NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA HAYAZUII MCHAKATO WA KATIBA MPYA KUENDELEA

 

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjGZkMUexifctjYEOHXo80LAsKeL5jAMJ34mJs1ceNri9P1MfH_L_7i0wPcnbER0khTAoQ3umUBbxzmTF4rfqb_vHZ8Hq1Z3B-pM3qfvfZvIHoWigfE7ObSRtTMJLWlTkxJChYGMsYXAxc/s1600/MMGM4299.jpg
Kamati kuu na halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi {NEC} zimekutana mjini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine vikao hivyo vimejadili mchakato wa bunge la katiba na kubainisha mafanikiano ya upatikanaji wa katiba mpya kati ya Rais Jakaya Kikwete na vyama vya siasa vinavyiunda kituo cha Demokrasia Tanzania {TCD} hayazuii chama hicho kuendelea na mchakato wa katiba.
 
Vikao hivyo vikuu vya CCM katika ngazi za mbali na kujadili mchakato wa bunge maalum la katiba pia vimezungumzia mustakabali wa chama hicho katika chaguzi zijazo za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu huku katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho Nape Nauye akisema wataendelea kujadili katiba kwani ajenda za TCD sio ajenda za CCM kwa kuwa vikao vyake vinajitegemea na viko huru.
 
Akizungumzia msimao wa chama hicho kuhusu kura za maoni ya wananchi Nape amesema CCM itaendelea kuheshimu sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2012 sura ya 83 inayoelekeza kura za maoni zipigwe ndani ya siku 84 baada ya bunge maalum kuvunjwa lakini pia akisisitiza sheria hiyo inaweza kufanyiwa mabadiliko na bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright 2025 EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG | Designed By Code Nirvana
Back To Top