askari wa
ulinzi shirikishi, wamefanikiwa kufumua danguro hatari linaloendesha
shughuli zake katika eneo la shule baada ya kumnasa mwanamke aliyedai ni
mke wa mtu akifanya uzinzi na njemba ambaye hakujulikana jina
lake. Kikosi cha OFM kimkurupusha mke wa mtu aliyekuwa akifanya uzinzi
na njemba moja(jina halikufamika). Tukio hilo la aibu ya karne lilijiri
ndani ya eneo la shule ya msingi Shekilango, iliyopo Mapambano, Sinza
jijini Dar, hivi karibuni ambapo mke huyo wa mtu alikuwa akichepuka.
Awali, OFM ilipokea taarifa za kuwepo kwa uchafu huo kutoka kwa
wasamaria wema wanaoishi eneo hilo baada ya kukerwa na tabia hiyo chafu
huku wakiacha kondom zikiwa zimezagaa na kuhatarisha afya za watoto wao
ambao huchezea mipira hiyo ya kinga kama mapulizo.
Baada ya
OFM kunyetishiwa ishu hiyo, walishirikiana na askari hao ambapo
walivamia eneo hilo na kumbamba mwanamke huyo akibanjuka na njemba.
Wazinifu
wakivaa mara baada ya kunaswa wakifanya yao. Wawili hao, baada ya
kubambwa 'laivu' walitiwa kizuizini kabla ya vijana wanaodaiwa kuchukua
posho kwa wanaofanyia mambo yao kwenye danguro hilo kuanzisha vurumai
ingawa walidhibitiwa huku jamaa aliyekuwa anahudumiwa akitoka nduki.
Akizungumza
na gazeti hili, mwanamke huyo aliomba asamehewe na kusema kwamba
kinachomsababishia kufanya shughuli hiyo ni ugumu wa maisha na kundi la
watoto anaowalea ambao baba yao hana ajira.
Wazinifu
wakiwa chini ya ulinzi wa Makamanda wa OFM. Gazeti hili lilipotaka
kuzungumza na mumewe ili kujua kama anafahamu kuwa mkewe anafanya
biashara haramu ya kuuza mwili, mwanamke huyo alidai kwamba mumewe hana
simu.
Mmoja wa
mashuhuda wa tukio hilo alisikika akisema: "Dah! Mngewahi dakika kumi
tu, mngemkuta baba wa Kiarabu aliyeingia na mwanamke muda si mrefu, hili
danguro linatumiwa usiku kucha, yaani linapoingia giza tu hapa ni balaa
hadi asubuhi."
Mwalimu
wa zamu, Kilavo Charles, aliiambia OFM kuwa suala hilo limeshafikishwa
kituo cha Polisi Mabatini ambao waliahidi kulishughulikia.“Ni aibu,
asubuhi watoto wanafagia kondom, tunakosa cha kuwaambia, hii ni hatari
kwa kweli na tunaomba mamlaka zinazohusika zilifanyie kazi jambo hili,”
alisema.
Post a Comment