Watu watatu wamepoteza maisha na
wengine 6 wako katika hali mbaya kati ya majeruhi 17 wa ajali ya moto
uliosabishwa na watu waliokuwa wakiiba mafuta baada lori lililokuwa
limebeba shehena ya mafuta ya Petroli kuanguka karibu na makazi ya watu
eneo Mbagala charambe jiji Dar es salaam.
Mwandishi wetu amefika katika eneo hilo na kushuhudia mabaki ya lori
lililokuwa limebeba mafuta ya Petroli huku maduka yaliyokuwa yamezunguka
nyumba ya kulala wageni yakiwa yameteketea kwa moto wa Petroli
uliosababishwa na baadhi ya watu waliokuwa wakiiba mafuta bada ya lori HILO
lililobeba mafuta kuanguka usiku wa kuamkia leo,ambapo inadaiwa miongoni
mwa waathirika hao alichomoa Betri ya lori hilo na kusababisha mlipuko
wa mafuta.
Kutokana na moto huo baadhi ya wafanyabiashara waliopoteza mali zao
ambapo wengine mpaka sasa hawajajua thamani ya mali zililotekea ambapo
mmoja wa wafayabiashara Bwana Ali Mohamed mmiliki wa duka la vifaa vya
ujenzi amedai kupoteza malizenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni
70, huku wengine wakitaka bima ya lori itumike kufidia mali
zilizopotea.
Akielezea tukio lilivyotokea mmoja wa wagonjwa Bwana Rajabu
Selemani amesema baadhi ya watu walioungua akiwemo yeye alikuwa anapita
barabarani akitokea kazini ndipo alipokuta barabara imetapakaa mafuta ya
petroli na baadae moto mkali ghafla ukaanza kuwaka na kuwaunguza
miguuni.
Muuguzi wa zamu wa hospitali ya temeke, Bi Rolesta Kinonda amesema
hospitali wamepokea maiti 1 ya mwanaume, majeruhi 20, 19 wanaume na
mwanamke ambapo kati ya majeruhi hao wanne wamewabakiza hospitali hapo
na mwanamke ameruhusiwa baada ya kupata huduma ya kwanza.
Akizungumizia tukio hilo baada ya kutembelea wagonjwa katika
hosptali ya taifa ya muhimbili na hospitali ya temeke, mkuu wa mkoa wa
dar es salaam Bwana Said Mecky Sadiki amewataka wananchi wasilikimbile
kuiba mafuta wakati malori ya mafuta yanapoanguka.
credits:itv
Post a Comment