Timu
ya England imefanikiwa kupata ushindi mara mbili katika michezo miwili
ya kundi E ya kufuzu kucheza michuano ya bara la Ulaya ya mwaka 2016
baada ya kupata ushindi mnono wa 5-0 dhidi ya San Marino.
England
alianza kuvuna magoli kupitia kwa mlinzi wake Phil Jagielka aliyefunga
katika dakika ya 24 kwa mpira wa kichwa kabla ya Wayne Rooney kuongeza
bao la pili kwa njia ya penalti katika dakika ya 43 kutoka na madhambi
ya mchezaji wa San Marino Andy Selva.
Naye
mshambuliaji Danny Welbeck alifanikiwa kutumbukiza goli la tatu kwenye
dakika ya 49. Goli hili lilitokana na mpira wa pasi kutoka kwa mchezaji
mwenzake wa Arsenal ambaye aliingia kipindi cha pili Alex
Oxlade-Chamberlain.
Andros
Townsend aliiongezea timu yake ya England goli la nne kwa mkwaju wa
mbali kabla ya Alessandro Della Valle kujifunga mwenyewe kutokana na
kugongwa na mpira uliopigwa na Rooney.
Matokeo
ya michezo mingine: Belarus 0: Ukaraine 2, Macedonia 3: Luxembourg 2,
Slovakia 2: Spain 1, Lithuania 1:Estonia 0, Slovenia 1: Switzerland 0,
Liechtenstein 0: Montenegro 0, Moldova 1:Austria 2, Sweden 1: Russia 1 BBC
Post a Comment