Msanii mkongwe wa filamu Bongo Issa Musa ‘Cloud’.
MSANII mkongwe wa filamu Bongo Issa Musa ‘Cloud’ amekana tuhuma
zinazosambazwa mtandaoni kuwa alimfitini muigizaji mwenzake, Mohammed
Mwikongi ‘Frank’ ili kumzuia asisafiri kuelekea Uingereza miezi michache
iliyopita.“Mimi sikumfitini Frank, yule mtu alinifuata mwenyewe kwa
makubaliano ya mdomo kuwa nikacheze filamu, sikuwa peke yangu,
tuliongozana na kina Monalisa na Riyama, tatizo ni la huyo aliyenipeleka
kule, nilifanya mambo kwa mazoea na ndiyo sababu anaamua kusambaza
uongo dhidi yangu,” alisema mkongwe huyo
Msanii mkongwe wa filamu Mohammed Mwikongi ‘Frank’.Aliwasihi wasanii
wenzake nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wahakikishe wanaingia
mikataba ya maandishi ili wawe na ushahidi wakati waliokubaliana nao
kazi wanapoleta ujanjaujanja kama ilivyomtokea yeye katika safari hiyo
ya Uingereza ambayo sasa inamletea uadui na Frank.
Post a Comment