Rais
Uhuru Kenyatta wa Kenya (kushoto) akilakiwa na Makamau wa Rais, William
Ruto alipowasili JKIA leo alfajiri akitokea The Hague.
Rais Kenyatta akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea leo alfajiri.
RAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya, leo alfajiri amepokelewa kishujaa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi akitokea The Hague, Uholanzi.
Rais
Kenyatta alienda katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), The
Hague anapokabiliwa na mashtaka ya kupanga utekelezaji wa mauaji ya
kikabila yaliyopelekea kuuawa kwa zaidi ya 1,200 baada ya uchaguzi wa
urais wa mwaka 2007.
Wakenya
kutoka sehemu mbalimbali za taifa hilo wamekusanyika JKIA kuanzia
majira ya saa 9 alfajiri kumsubiri Rais Kenyatta aliyekuwa ameambatana
na mkewe Margaret Kenyatta.
Makamau wa Rais, William Ruto ndiye aliyeongoza viongozi wa serikali na kitaifa kumpokea mkuu huyo wa nchi.
Ndege
iliyombeba Rais Kenyatta na viongozi alioambatana nao imetua JKIA saa
12:40 alfajiri na baadaye rais huyo alipokelewa kwa burudani za
kitamaduni kutoka makundi mbalimbali ya sanaa.
PICHA: FACEBOOK
Post a Comment