Katika
hali isiyo ya kawaida wakazi wa manispaa ya Singida wameingiwa na
taharuki na kuanza kukimbia ovyo baada fisi kuonekakana katikati ya mji
wa Singida akiwa anakimbia na kuingia katika maduka ya wafanya
biashara.
Wakieeleza kwa hisia tofauti baadhi ya wakazi huku wengine wakiwa
wamepanda juu ya mapaa ya nyumba pamoja na watoto wao kwa hofu ya
kuumwa,wamesema kuonekana kwa fisi mjini katikati ni jambo la ajabu
kwani wanyama kama hao honekana vijiji au porini,wengine wamesema labda
mnyama huyo amechelewa kurudi vichakani wakati alipokuwa amekuja kula
mabaki ya chakula mjini.
Akielezea
tukio hilo Afisa maliasili mkoa wa Singida Bwana Charles
Kidua amesema pamoja na kwamba wanyama kama fisi wapo katika manispaa ya
Singida na pindi wanapo onekana katika maeneo ambayo siyo ya kawaida
,Basi wananchi watoe taarifa kwa mamlaka husika kwani wanyama kama haho
wana weza kuwa na ugonjwa wa kichaa ,badala ya kujichukulia hatua
mkononi ya kuwaua.
Kutokana na umati wa wananchi kuwa wengi wakati wakimfukuza fisi
huyo bila kujali askari waliokuwa wakituliza fujo huku wakiwa na
silaha,wanachi walifanikiwa kuwapokonya askari fisi baada ya kumtega na
kamba huku wakiimba tunataka fisi wetu na kuamua kumkimbiza mjini huku
wakimpiga umbali wa kilomita mbili.
Post a Comment