
Ajali hiyo mbya imetokea katika eneo hilo la pida katika barabara kuu ya Mwanza-Sirari wakati gari hilo likitokea jijini Mwanza kwenda Nyamongo wilayani Tarime, ambapo imeelezwa kuwa baada ya kugongwa kwa mwanafunzi huyo Keneth Barnaba dereva wa gari alijitahidi kuwakwepa wanafunzi wengine lakini kutokana na mwendo kasi gari hilo lilimshinda na kupaa juu kisha kuvamia jengo la mashine ya kusagia nafaka na nyumba ya familia moja kijijini hapo.
Wakizungumza wakati wa maandalizi ya mazishi ya mwanafunzi huyo baadhi ya wananchi wa kijiji hicho, wameiomba wakala wa kuhudumia barabara nchini Tanroads mkoa wa Mara kuangalia uwezekano wa kuweka matuta katika eneo hilo ili kuzua ajali hizo za mara kwa mara.
Post a Comment