Hussein
Makame-MAELEZO
JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekanusha vikali uvumi unaoendelea
kuzushwa jijini Dar es Salaam kuhusu utekeaji nyara wa watoto wadogo wanaosoma
shule za jiji hilo na kuwataka wananchi kuupuuza.
Akizungmza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova,
alisema kuwa
mpaka sasa jeshi hilo halina taarifa yoyote ya mtoto kutekwa au kufanyiwa
madhara yoyote kwa mtindo wa utekaji nyara.
“Jeshi la Polisi limegundua kwamba huu ni uvumi
ambao haujulikani chanzo chake hivyo wananchi
wanaombwa kuachana nao na kuupuza kwani unaleta hofu katika jamii bila sababu
za msingi” alisema Kova.
Alisema kuwa pia uvumi huo umeanza kuleta
usumbufu ambapo mnamo Oktoba 3 mwaka huu
saa 3:00 asubuhi huko Vingunguti, mtu mmoja aitwaye Prosper Makame (34) akiwa
na mkewe Marystella Munis (30) walipata usumbufu unaotokana na uvumi huo.
Kamishna Kova aliongeza kuwa watu hao ambao
ni wafanyabiashara wa vyombo vya nyumbani
walifika maeneo ya shule ya msingi Kombo iliyopo Vingunguti kwa ajili ya
biashara zao, wakiwa na gari aina ya Noah yenye namba T252 DAY, ghafla walizingirwa na watu
wakidaiwa wanateka wanafunzi.
“Pia mnamo Oktoba 13, 2014 majira ya saa 4:00
asubuhi huko katika kituo cha Polisi Tabata uliibuka uvumi kuwa gari namba T548
BUN aina ya Noah rangi nyeusi ambayo ni mali ya askari polisi A/INSP Ester wa
kikosi cha usalama barabarani, ilivumishwa kwamba ndani ya
gari hiyo kuna vichwa vitano vya watoto wa shule ya msingi Mtambani na
kusababisha wazazi wenye watoto wanaosoma shule hiyo kukusanyika kituoni hapo
ili kushuhudia na kuona vichwa hivyo” alisema Kamishna Kova na kuongeza:
“Na
ndipo Mkuu wa kituo hicho cha Polisi
aliamuru gari hilo lifunguliwe na kuwathibitishia wananchi kuwa habari hizo ni
za uongo na uvumi”
Kutokana
na tukio hilo jeshi hilo lilifanya uchunguzi na kumkamata mtu mmoja Gilbert
Stanley (32) mhehe mkulima na mkazi wa Tabata alipohojiwa alikiri kueneza
habari hizo na kudai yeye aliambiwa na mtu ambaye hakumkumbuka.
Hivyo,
Kamishna Kova alisisitiza kuwa uvumi wa kuwepo kwa kikundi cha wahalifu
wanaowateka watoto wanafunzi si wa kweli hata kidogo na hivyo wananchi
wanatakiwa kuepukana na taarifa hizo kwani zinaweza kusababisha uvunjifu wa
amani.
Katika hatua nyingine, Kamishna Kova alithibitisha kutokea kwa vifo
vya watu watano na wengine 16 kujeruhiwa katika ajali ya moto iliyotokea Oktoba
13 mwaka huu majira ya saa 5:00
usiku huko kwenye mzunguko waMbagala
Charambe baada ya lori aina ya Scania
T347 BXG lilipoanguka likiwa na mafuta aina ya petrol lita 38,000.
Aliwataja
waliofariki kuwa ni Masoud Masoud mkazi wa Charambe, Hassani Mohamed mkazi wa
Mbagala Kibangulile, Mohamed Ismail, Ramadhani Halfan na Maulidi Rajabu wote ni
wakazi wa Mbagala Charambe.
Alisema kuwa majeruhi wamelazwa kwenye hospitali
ya taifa ya Muhimbili na hospitali ya wilaya ya Temeke wakiendelea na matibabu
huku ajali hiyo pia ikisababisha nyumba ya kulala wageni iitwayo United kuungua
moto na kuteketea kwa pikipiki saba za bodaboda zilizokuwa zimeegeshwa karibu
na aneo hilo, maduka matano yenye bidhaa zenye thamani ya shilingi
Milioni 197 yaliungua moto.
Kamishna Kova aliwataka wananchi kuacha tabia ya
kukimbilia kwenye ajali za magari ya mafuta kwani ni hatari kwa maisha yao
kwani watu wengi waliojeruhiwa walikuwa wakichota mafuta
yaliyomwagika kutokanana ajali hiyo.
Katika tukio lingine, Kamishna Kova alisema kuwa Jeshi hilo
limefanikiwa kumkamata jambazi sugu aitwaye Paulo Thamas Milanzi maarufu
Chinga (35) mmakonde mkazi wa Chanika
ambaye baada ya majibizano ya risasi jambazi hilo lilijeruhiwa na kufikshwa
hospitali ya muhimbili kwa matibabu ingawa baadaye alifariki dunia.
Alisema jambazi hilo lilikuwa likitafutwa na polisi
kutokan na kuhusika kwenye matuio ya mauaji na wizi ikiwemo tukio la kuuawa kwa
Afisa Mwandamizi wa Usalama wa Taifa, Sylivabus Adrian Mzeru Aprili 29 mwaka
huu liliotokea
Uwanja wa Ndege.
Aliongeza
kuwa jambazi lilikamatwa na bastola aina ya Star ambapo majambazi wenzake
walikamatwa na sasa wako gerezani, hivyo ameitahadharisha jamii iachane na
uhalifu kwani hauna manufaa yoyote.
Post a Comment