Mkutano
Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) utafanyika Novemba 15 mwaka
huu jijini Dar es Salaam ambapo moja ya ajenda ni uchaguzi mdogo wa
kujaza nafasi moja ya uongozi kwenye bodi hiyo.
Nafasi
hiyo ya ujumbe kwenye Kamati ya Uendeshaji ya TPLB iliyokuwa
ikishikiliwa na Kazimoto Muzo imebaki wazi baada ya klabu yake ya Pamba
ya Mwanza kushuka daraja kutoka la Kwanza hadi la Pili.
Hivyo,
wagombea wa nafasi hiyo ni kutoka kwenye klabu za Ligi Daraja la Kwanza
(FDL). Klabu hizo zina nafasi mbili kwenye Kamati ya Uendeshaji ya TPLB
ambapo nyingine inashikiliwa na Omari Mwindadi wa klabu ya Mwadui ya
Shinyanga.
*SDL WAONGEZEWA MUDA WA USAJILI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeongeza muda wa usajili wa
wachezaji kwa timu za Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa siku saba ambapo
sasa utamalizika Oktoba 21 mwaka huu.
Awali
usajili huo unaofanyika kwa njia ya mtandao (online) ulikuwa umalizike
jana (Oktoba 14 mwaka huu), lakini ni klabu chache ndizo zilizoweza
kusajili ndani ya muda uliopangwa.
Klabu
ambazo hazijakamilisha shughuli hiyo ya usajili, zinatakuwa kukamilisha
ndani ya siku hizo saba kwani TFF haitaongeza tena muda wa usajili.
Vilevile klabu za SDL zinakumbushwa kuwasilisha majina ya viwanja vya
nyumbani ambavyo timu zao zitatumia kwenye ligi hiyo.
TFF ilifanya mafunzo ya usajili kwa maofisa usajili wa klabu hizo Oktoba 6 na 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Timu
za SDL zimegawanywa katika makundi manne ya timu sita zitakazocheza
ligi kwa mtindo wa nyumbani na ugenini. Kundi A lina timu za Mpanda
United ya Katavi, Ujenzi (Rukwa), Mvuvumwa FC (Kigoma), Mji Mkuu FC
(Dodoma), Milambo (Tabora) na Singida United (Singida).
Kundi
B ni Mbao FC (Mwanza), Bulyanhulu FC (Shinyanga), Eleven Stars
(Kagera), JKT Rwamkoma (Mara), Pamba (Mwanza) na AFC (Arusha). Kundi C
ni Navy, Mshikamano, Transit Camp na Abajalo za Dar es Salaam, Kiluvya
United (Pwani) na Kariakoo (Lindi(.
Timu
zinazounda kundi D ni Magereza (Iringa), Town Small Boys (Ruvuma),
Njombe Mji (Njombe), Volcano FC (Morogoro), Wenda FC (Mbeya) na Mkamba
Rangers (Morogoro).
*MAREKEBISHO YA RATIBA FDL KUNDI A
Mechi
nne za Kundi A la Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zimefanyiwa marekebisho
ili kutoa fursa ya matumizi ya Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar
es Salaam.
Timu
za African Lyon na Kimondo FC ambazo awali zilikuwa zicheze Oktoba 25
mwaka huu kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, sasa zitacheza Oktoba
26 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Nayo
mechi ya Polisi Dar es Salaam na Majimaji ya Songea iliyokuwa ichezwe
Oktoba 26 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, sasa itachezwa
Oktoba 27 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
Mechi
ya Friends Rangers na Ashanti United iliyokuwa ichezwe Mabatini mkoani
Pwani, Oktoba 26 mwaka huu, sasa itachezwa Uwanja wa Karume, Oktoba 28
mwaka huu.
Pia
mechi ya Lipuli FC na JKT Mlale iliyokuwa ichezwe Oktoba 25 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa, imesogezwa mbele kwa siku moja.
Mechi hiyo sasa itachezwa Oktoba 26 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
Post a Comment