SHIRIKISHO LA WANAFUNZI WA VYUO VYA ELIMU YA JUU
UNAUNDWA KWA MUJIBU WA KATIBA YA CHAMA CHA
MAPINDUZI YA MWAKA 1977 TOLEO LA 2012 ,SEHEMU YA
TATU,IBARA 31 (1) C
UTANGULIZI
Chama cha Siasa kikomavu hakitaacha kuunda Shirikisho la Wanafunzi
wa vyuo vya elimu ya juu na kuufanya uhusiano wake kuwa wa chanda
na pete. Umadhubuti wa chama chochote cha siasa, ufanisi wake na
uhai wake, unategemea vijana wake na hasa vijana waliopo katika vyuo
vya elimu ya juu. Hivyo, Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya
juu unapaswa kuwa imara kimuundo,kimaadili na kimkakati. Umadhubuti
huo hutoa msaada mkubwa katika kufanikisha azma na malengo ya
chama cha siasa.
Kwa hivyo, Shirikisho la Wanafunzi wa Tanzania wa vyuo vya elimu ya
juu,umeanzishwa kwa kuzingatia umuhimu wa Chama kuungwa mkono
na kundi la Vijana Wasomi waliopo katika Taasisi za Elimu ya Juu hapa
nchini. Lengo kuu likiwa ni kuwapatia wanafunzi wa elimu ya juu fursa
ya kukutana na kubadilisha mawazo na uzoefu juu ya maswala ya Itikadi
ya chama,maadili na uzalendo wa nchi pamoja na kujenga fikra za
kujitegemea na ubunifu.
Shirikisho la Wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania tunatambua kuwa
harakati za kuleta mapinduzi ya kiuchumi,kisayansi na kitekinolojia na
kujenga jamii ya watu iliyo sawa nchini Tanzania, tunahitaji chombo
madhubuti kinachounganisha fikra na vitendo vya vijana wote wakiwemo
vijana wasomi.
Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu tunaounda,unakusudia
kushiriki katika kutatua changamoto za wanavyuo zinazohusu elimu,
mikopo ya elimu ya juu, siasa, namna bora ya kujiajiri na uwezeshaji.
Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu tutaratibu na kukuza
uhusiano na ushirikiano baina yake na taasisi za hiari zinazojishughulisha
na maswala ya elimu,sayansi na utamaduni ndani na nje ya Tanzania.
Msingi wa elimu ni kumfanya mtu aweze kujitambua na wakati huo huo
aweze kujitawala. Elimu humsaidia mtu kugundua uwezo wake na
mipaka yake. Aidha, humuonesha jinsi ya kuondokana na mambo ovyo
aliyoyarithi na jinsi ya kutumia vipaji vyake ili kuendesha maisha yake
hapo elimu itakuwa imefanikiwa kutimiza malengo yake.
Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu tunazingatia kwamba
elimu ndiyo rasilimali kuu ya taifa letu. Tunakubali kimsingi kwamba ili
tuweze kupata elimu bora wanafunzi tunalazimika kuwa na nidhamu, ya
hali ya kuwa na silka ya uchunguzaji, ili uelewa mpana wenye
kuyafahamu mazingira aliyopo.
SEHEMU YA KWANZA
JINA, IMANI NA MADHUMUNI
Ibara ya 1 Jina litakuwa “Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo
vya elimu ya juu Tanzania”
Ibara ya 2
Makao Makuu
Makao Makuu ya Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya
elimu ya juu ni Dar es salaam, na kutakuwa na Ofisi
Ndogo Dodoma na Zanzibar.
Ibara ya 3
Alama
Alama ya Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya
juu itakuwa ni “ GURUDUMU LA MAENDELEO “
Ibara ya 4
Kauli
Kauli ya Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya
juu ni:
“ELIMU NA MAENDELEO YA WATU”
FUNGU LA KWANZA - IMANI
Ibara ya 5
Imani
Imani ya Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya
juu ni: “Elimu ya juu ndiyo nguvu ya maendeleo.”
FUNGU LA PILI – MADHUMUNI NA MALENGO
Ibara ya 6
Madhumuni na Malengo
Madhumuni ya Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya
elimu ya juu itakuwa kama ifuatavyo:-
i. Kushughulikia uratibu wa masuala ya
Wanafunzi wa Vyuo vya elimu ya juu kupitia
Matawi yao ambayo lazima yawe nje ya
maeneo ya vyuo.
ii. Kusimamia na kufuatilia harakati za kisiasa
na za kitaaluma za Wanafunzi wa Vyuo
vya elimu ya juu.
iii. Kuwa kiungo kati ya Shirikisho la vyuo vya
elimu ya juu na Vikao vya Chama vya
Kitaifa kupitia Sekretariet ya Halmashauri
Kuu ya CCM ya Taifa.
iv. Kusimamia shughuli za Uchaguzi wa
Viongozi katika Shirikisho la Wanafunzi
wa vyuo vya elimu ya juu,na Uchaguzi wa
Uwakilishi kupitia vyombo vya dola.
v. Kusajili wanafunzi katika matawi ya vyuo
kwa shabaha ya kuwa na wanachama kwa
kadiri inavyowezekana.
vi. Kushiriki mikutano, midahalo na
makongamano kwa ajili ya kuwajenga
wanavyuo wawe na uwezo wa kujiamini
kuhusu nchi yao na nafasi ya CCM.
FUNGU LA TATU - MAJUKUMU
Ibara ya 7
Majukumu ya Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
Kwa hiyo Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya
juu utakuwa na majukumu yafuatayo;
i. Kuwajenga wanafunzi katika maadili ya uzalendo,
umoja na utaifa. Pia kuthubutu kutenda
katika mazingira ya maendeleo ya sayansi
na teknolojia.
ii. Kuunga mkono na kushiriki kikamilifu katika
ukuzaji na uendelezaji wa vipaji na taaluma
za wasomi kwa lengo la kuimarisha moyo
wa uvumbuzi miongoni mwa jamii ya vijana
wasomi wa Taifa.
iii. Kukuza uhusiano na ushirikiano baina ya
Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu
ya juu na taasisi za hiari zinazojishughulisha
na masuala ya elimu,sayansi na utamaduni
ndani na nje ya Tanzania.
iv. Kuwa chemchem ya fikra na mawazo ya
kimaendeleo kwa taifa.
v. Kufanya tafiti za changamoto zinazoikabili
taifa.
SEHEMU YA PILI
UANACHAMA NA UONGOZI
FUNGU LA KWANZA - UANACHAMA
Ibara ya 8
Wanachama
Kila mwanafunzi anayetimiza masharti
ya kujiunga na chuo husika na
kujiandikisha katika Tawi la Chuo
atakuwa mwanachama katika Matawi ya
vyuo hata kama atakuwa hajapata kadi
ya chama.
Ibara ya 9
Masharti ya Uanachama
Mwanafunzi atakayekubaliwa kuwa
mwanachama katika tawi awe na tabia
nzuri kwa vitendo vyake na kauli yake,
kuwa mwaminifu,mwadilifu na
mzalendo.
Ibara ya 10
Utaratibu wa Kuomba, Kufikiriwa Uanachama, Mafunzo,
Kiingilio na Ada za Uanachama.
Mwanafunzi yeyote anayetaka kuwa
mwanachama wa CCM na kupata kadi
ya chama itakuwa kama ilivyoainishwa
katika Katiba ya CCM sehemu ya pili
fungu la kwanza ibara ya 9,10,na 11.
Mtu akikubaliwa kuwa
mwanachama itabidi atekeleze masharti
ambayo yameainishwa katika Katiba ya
CCM sehemu ya pili Fungu la kwanza
Ibara ya 12 (1).
Ibara ya 11
Kuondoka katika Shirikisho la vyuo vya elimu ya juu
Mwanafunzi ambaye ni mwanachama,
unachama wake utakoma ndani ya
Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya
elimu ya juu iwapo;
i. Ataacha kwa hiari yake
ii. Ataachishwa
iii. Atahitimu masomo yake.
Kila mwanachama atakuwa na haki zifuatazo:
Ibara ya 12
Haki za mwanachama
Haki za mwanachama zitakuwa kama
ilivyoainishwa katika Katiba ya CCM sehemu ya
pili Fungu la 1 ibara ya 14 (1), (2),(3),(4) na (5).
Ibara ya 13
Wajibu wa Mwanachama
Kila mwanachama atakuwa na wajibu kama
ilivyoainishwa na Katiba ya CCM sehemu pili
fungu la kwanza ibara ya
15(1),(2),(3),(4),(5),(6),(8) na (9).
FUNGU LA PILI – VIONGOZI
Ibara ya 14
Maana ya Kiongozi, Sifa za Kiongozi, Miiko
ya Kiongozi, Kuondoka katika uongozi na
Kiwango cha Kura katika Uchaguzi wa Kiongozi.
Mambo haya yote yatakuwa kama yalivyoainishwa
na Katiba ya CCM sehemu ya pili fungu la pili ibara
ya 16, 17, 18, 19 na 20.
Kiongozi sharti awe na sifa mbili: kwanza, awe
na kadi ya chama na awe Mwanafunzi wa vyuo
vya elimu ya juu nchini.
Ibara ya 15
Kuondoka katika Uongozi.
Kutakuwa na aina zifuatazo za kuondoka katika
uongozi wa Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya
elimu ya juu kama zilivyoainishwa katika ibara ya 11
ya Kanuni hizi.
Ibara ya 16
Muda wa Uongozi
Kiongozi yeyote wa Shirikisho la Wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu aliyechaguliwa kwa mujibu
wa Kanuni hizi atashika madaraka yake kwa
muda wa miaka mitatu ya uongozi.
SEHEMU YA TATU
VIKAO VYA SHIRIKISHO LA WANAFUNZI WA VYUO VYA ELIMU
YA JUU FUNGU LA KWANZA – VIKAO VYA MATAWI
Ibara 17
Vikao vya Tawi
Kutakuwa na vikao vifuatavyo vya Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu katika kila
Tawi:-
i. Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Tawi
ii. Kamati ya Siasa ya Tawi
Ibara ya 18 (a)
Mkutano wa
Halmashauri Kuu
ya Tawi
Kutakuwa na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Tawi
katika kila Tawi la Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo
vya elimu ya juu, ambao litakuwa na wajumbe
wafuatao:-
i. Mwenyekiti wa Tawi
ii. Katibu wa Tawi
iii. Katibu Siasa na Uenezi wa Tawi
iv. Katibu wa Uchumi na Fedha wa Tawi
v. Katibu wa Uhamasishaji wa Tawi
vi. Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Tawi
vii. Mlezi wa Tawi (ambaye hatashiriki kupiga
kura katika Kikao chochote).
viii. Wanachama wote ambao ni wanafunzi wa
chuo wa Tawi hilo.
(b) Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Tawi wa Shirikisho
la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ndicho kikao
kikuu cha Tawi.
(c) Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Tawi utafanyika
angalau mara moja kila muhula wa masomo na si
chini ya mara mbili kwa mwaka wa masomo.
(d) Mwenyekiti wa Tawi ndiye atakayeongoza Mkutano
wa Halmashauri Kuu ya Tawi. Mwenyekiti
asipokuwepo Katibu ataongoza.
Ibara ya 19
Kazi za Mkutano
wa Halmashauri
Kuu ya Tawi
Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Tawi ndicho kikao
cha juu katika Tawi.
(a) Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Tawi
utafuatilia, utajadili, mafanikio na changamoto
katika mambo yanayohusu masilahi ya
wanafunzi wa elimu ya juu. Mambo hayo ni
elimu,mikopo kwa ajili ya elimu ya juu,siasa
na uwezeshaji pamoja na masuala ya Kitaifa.
(b) Utajadili taarifa ya kazi za Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu katika
Tawi na kutoa mapendekezo ya utekelezaji
wa siasa za Tawi kwa Kamati ya Siasa ya
Tawi. Utapima mafanikio ya utekelezaji wa
maazimio ya mikutano yake iliyopita pamoja
na yale ya vikao vya juu.
(c) Unapofika wakati wa uchaguzi, Mkutano wa
Halmashauri Kuu ya Tawi itafanya mambo
yafuatayo:-
i. Utamchagua Mwenyekiti wa Tawi
ambaye atashika nafasi hiyo ya uongozi
kwa mujibu wa ibara ya 16 ya kanuni
hizi. Pamoja na Katibu wa Tawi,Katibu
wa Siasa na Uenezi wa Tawi,Katibu wa
Uchumi na Fedha wa Tawi,na Katibu wa
Uhamasishaji wa Tawi.
ii. Utajaza nafasi wazi za uongozi
zinazotokea katika Tawi.
(d) Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Tawi
utafanyika mara moja kila muhula wa
masomo lakini unaweza kufanyika wakati
wowote endapo itaagizwa kufanya hivyo na
kikao kingine cha ngazi ya juu.
Ibara ya 20
Kikao cha Kamati
ya Siasa ya Tawi
Kutakuwa na Kikao cha Kamati ya Siasa ya Tawi,
kwa kila Tawi la vyuo vya elimu ya juu.
a) Kikao cha Kamati ya Siasa ya Tawi
kitakuwa na wajumbe wafuatao;
i. Mwenyekiti wa CCM wa Tawi
ii. Katibu wa CCM wa Tawi
iii. Katibu wa Siasa na Uenezi wa
Tawi.
iv. Katibu wa Uchumi na Fedha wa
Tawi.
v. Katibu wa Uhamasishaji wa
Tawi.
vi. Wajumbe watano
waliyochaguliwa na
Halmashauri Kuu ya Tawi
kutoka miongoni mwao.
vii. Mwenyekiti wa Tawi wa kila
Jumuiya ya Wananchi
inayoongozwa na CCM iliyopo
katika Tawi.
b) Kikao cha Kamati ya Siasa ya Tawi
kitafanya mikutano yake mara moja
kila baada ya miezi miwili.
c) Mwenyekiti ataongoza Kikao cha
Kamati ya Siasa ya Tawi.
Mwenyekiti asipokuwepo Katibu
ataongoza kikao husika.
Ibara ya 21
Kazi za Kikao
cha Kamati ya
Siasa ya Tawi
Kazi za Kikao cha Kamati ya Siasa ya Tawi zitakuwa
kama zifuatazo:
(a) Kulinda na kutetea maslahi ya
wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.
(b) Kutoa uongozi wa siasa katika eneo lake.
(c) Kuandaa mikakati ya kampeni za uchaguzi
na kampeni nyinginezo ndani ya Tawi na
nje ya Tawi.
(d) Kuelimisha fursa za ajira na kujiajiri na
uwezeshaji kwa wanafunzi wa vyuo.
(e) Kufanikisha elimu shirikishi na mafunzo
kwa wanafunzi na kuratibu semina na
midahalo ya uzalendo,maadili ya
taifa,elimu ya kujitegemea, uongozi na
ubunifu.
Unapofika wakati wa uchaguzi, Kamati ya Siasa ya
Tawi itashughulika na mambo yafuatayo;
i. Kufikiria na kutoa mapendekezo juu
ya wanachama wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
wanaoomba nafasi za Uongozi.
Mapendekezo hayo yatapelekwa kwa
Kamati ya Siasa ya Shirikisho la
Mkoa.
ii. Kupendekeza Mlezi wa Tawi kwa
Kamati ya Uratibu ya Shirikisho la
Taifa.
iii. Kikao cha Kamati ya Siasa ya Tawi
kitafanya mikutano yake kila baada
ya miezi miwili, lakini inaweza
kukutana wakati wowote
itakapoonekana inafaa.
iv. Kikao cha Kamati ya Siasa ya Tawi
kitaandaa Mkutano wa Halmashauri
Kuu ya Tawi.
13 | P a g e “ e l i m u n a m a e n d e l e o y a w a t u ”
Ibara ya 22
Wakuu wa Tawi
Kutakuwa na Viongozi Wakuu wa CCM wa Tawi
wafuatao;-
i. Mwenyekiti wa Tawi
ii. Katibu wa Tawi
iii. Katibu wa Siasa na Uenezi wa Tawi
iv. Katibu wa Uchumi na Fedha wa Tawi
v. Katibu wa Uhamasishaji wa Tawi.
Ibara ya 23
Mwenyekiti wa
CCM wa Tawi
Mwenyekiti wa Tawi atachaguliwa na Mkutano wa
Halmashauri Kuu ya Tawi na atakuwa katika nafasi
hiyo ya uongozi kwa mujibu wa ibara ya 16 ya
kanuni hizi.
Atakuwa na madaraka na kazi kama ilivyoainishwa
katika Katiba ya CCM ya mwaka 1977 ibara ya 43
(2),(3) na (4).
Ibara ya 24
Katibu wa CCM
wa Tawi
(a) Katibu wa Tawi atachaguliwa na Mkutano wa
Halmashauri Kuu ya Tawi lake na atakuwa
katika nafasi hiyo ya uongozi kwa mujibu wa
ibara ya 16 ya kanuni hizi.
(b) Atakuwa na madaraka na kazi kama
ilivyoainishwa katika Katiba ya CCM ya mwaka
1977 ibara ya 44 (2),(3), na (4).
Ibara ya 25
Katibu wa Siasa
na Uenezi wa
Tawi
(a) Atachaguliwa na Mkutano wa Halmashauri
Kuu ya Tawi na atakuwa katika nafasi hiyo
kwa mujibu wa ibara ya 16 ya kanuni hizi.
(b) Atakuwa na madaraka na majukumu kama
yalivyoainishwa katika Katiba ya CCM ya
mwaka 1977 ibara ya 45.
Ibara ya 26
Katibu wa
Uchumi na
Fedha wa Tawi.
Ibara ya 27
Katibu wa
Uhamasishaji wa
Tawi
(a) Atachaguliwa na Mkutano wa Halmashauri
Kuu ya Tawi na atakuwa katika nafasi hiyo
kwa mujibu wa Ibara ya 16 ya kanuni hizi.
(b) Atakuwa na madaraka na majukumu kama
yalivyoainishwa katika Katiba ya CCM ya
mwaka 1977 Ibara ya 46.
(a) Atachaguliwa na Mkutano wa Halmashauri
Kuu ya Tawi na atakuwa katika nafasi hiyo
kwa mujibu wa Ibara ya 16 ya kanuni hizi.
(b) Atawajibika juu ya masuala yote yanayohusu
wanafunzi kama vile mambo ya elimu,
mikopo ya elimu ya juu, na uwezeshaji.
(c) Ataratibu na kuweka mazingira ya
ushirikishwaji wa vijana katika shughuli za
kujitolea za kijamii.
(d) Kuendeleza,kukuza na kusimamia shughuli za
utamaduni na michezo katika Tawi.
FUNGU LA PILI – VIKAO VYA SHIRIKISHO LA MKOA
Ibara ya 28
Vikao vya
Shirikisho la
Mkoa
Kutakuwa na vikao vifuatavyo katika Shirikisho la
Mkoa:
i. Mkutano Mkuu wa Seneti wa Shirikisho la
Mkoa
ii. Kamati ya Uratibu ya Shirikisho la Mkoa
Ibara ya 29
Mkutano Mkuu
wa Seneti ya
Shirikisho la
Mkoa.
(a) Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Seneti ya
Shirikisho la Mkoa ambao utakuwa na
wajumbe wafuatao:
i. Mwenyekiti wa Seneti wa Shirikisho la Mkoa
ii. Katibu wa Seneti wa Shirikisho la Mkoa
iii. Katibu wa Siasa na Uenezi wa Mkoa
iv. Katibu wa Uchumi na Fedha wa Mkoa
v. Katibu wa Uhamasishaji wa Mkoa
vi. Wajumbe wote wa Kamati ya Uratibu ya
Shirikisho la Mkoa.
vii. Viongozi Wakuu wote wa CCM wa kila Tawi.
viii. Mwenyekiti wa Tawi wa kila Jumuiya ya
Wananchi inayoongozwa na CCM iliyopo katika
Tawi hilo.
(b) Mkutano Mkuu wa Seneti wa Shirikisho la
Mkoa ndicho kikao kikuu cha Shirikisho la
Mkoa.
(c) Mkutano Mkuu wa Seneti wa Shirikisho la
Mkoa utafanyika mara moja kila baada ya
miezi kumi na mbili au itakapohitajika
kufanyika.
(d) Mwenyekiti wa Seneti wa Shirikisho la Mkoa
ataongoza Mkutano Mkuu wa Seneti wa
Shirikisho la Mkoa kama hayupo Katibu wa
Seneti wa Shirikisho la Mkoa ataongoza.
16 | P a g e “ e l i m u n a m a e n d e l e o y a w a t u ”
Ibara ya 30
Kazi za Mkutano
Mkuu wa Seneti
wa Shirikisho la
Mkoa.
Kazi za Mkutano Mkuu wa Seneti wa Shirikisho la
Mkoa zitakuwa kama ifuatavyo:-
(a) Kupokea na kujadili taarifa za kazi zilizotolewa
na Kamati ya Uratibu ya Shirikisho la Mkoa na
kutoa maelekezo ya utekelezaji wake kwa
kipindi kijacho.
(b) Kujadili mambo yote muhimu ya wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu kuhusu elimu,mikopo ya
elimu ya juu,uwezeshaji,na michezo.
(c) Kuandaa,kuweka na kuratibu taarifa muhimu
za wanafunzi makada waliyopo na
wanaomaliza vyuo kwa matumizi ya Chama na
Taifa.
(d) Kuhakikisha kwamba maazimio na maagizo
ya Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Taifa
yanatekelezwa ipasavyo.
(e) Aidha,unapofika wakati wa Uchaguzi, Mkutano
Mkuu wa Seneti wa Shirikisho la Mkoa
utashughulikia mambo yafuatayo:-
i. Utamchagua Mwenyekiti wa Seneti wa
Shirikisho la Mkoa,Katibu wa Seneti wa
Shirikisho la Mkoa,Katibu wa Siasa na
Uenezi wa Seneti wa Shirikisho la
Mkoa,Katibu wa Uchumi na Fedha wa
Seneti wa Shirikisho la Mkoa na Katibu
wa Uhamasishaji wa Seneti wa Shirikisho
la Mkoa. Wote hawa watashika nafasi
hizo za uongozi kwa mujibu wa ibara ya
16 ya kanuni hizi.
17 | P a g e “ e l i m u n a m a e n d e l e o y a w a t u ”
ii. Kuunda kamati mbalimbali kadri
itakavyoonekana inafaa.
iii. Mwenyekiti wa Seneti wa Shirikisho la
Mkoa ataongoza Mkutano Mkuu wa
Seneti wa Shirikisho la Mkoa lakini kama
Mwenyekiti hayupo Katibu wa Seneti wa
Shirikisho la Mkoa ataongoza.
iv. Mkutano Mkuu wa Seneti wa Shirikisho la
Mkoa wa kawaida utafanyika kila baada
ya miezi kumi na mbili. Lakini unaweza
kufanyika wakati wowote iwapo
itaonekana inafaa.
Ibara ya 31
Kamati ya
Uratibu ya
Shirikisho la
Mkoa.
(a) Kutakuwa na Kamati ya Uratibu ya Shirikisho
la Mkoa ambayo itakuwa na wajumbe
wafuatao:-
i. Katibu wa Seneti wa Shirikisho la Mkoa
ii. Katibu wa Siasa na Uenezi wa Shirikisho la
Mkoa
iii. Katibu wa Uchumi na Fedha wa Shirikisho
la Mkoa
iv. Katibu wa Uhamasishaji wa Shirikisho la
Mkoa
v. Katibu wa Tawi wa kila Jumuiya ya
wananchi inayoongozwa na CCM katika
Tawi hilo.
(b) Kamati ya Uratibu ya Shirikisho la Mkoa
itafanya mikutano yake ya kawaida mara moja
kila muhula wa masomo.
(c) Katibu wa Seneti wa Shirikisho la Mkoa
ataongoza mikutano yote ya Kamati ya
Uratibu ya Shirikisho la Mkoa na kama hayupo
atachaguliwa Mwenyekiti wa muda kutoka
miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Uratibu
18 | P a g e “ e l i m u n a m a e n d e l e o y a w a t u ”
wa Shirikisho la Mkoa.
Ibara ya 32
Kazi za Kamati
ya Uratibu wa
Shirikisho la
Mkoa
(a) Kazi za Kamati ya Uratibu wa Shirikisho la
Mkoa zitakuwa kama ifuatavyo:
i. Kusimamia na kufuatilia harakati za
kisiasa na za kitaaluma katika Shirikisho
la Mkoa.
ii. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa
shughuli za kuandaa
midahalo,makongamano na mijadala ya
wazi itakayowahusisha wanafunzi katika
kuchambua,kufafanua na kuelezea
masuala mbalimbali yanayohusu
mustakabali wa Taifa.
iii. Kusimamia utekelezaji wa maagizo
kutoka vikao vya juu yanayohusu
wanafunzi. Aidha,kuratibu zoezi la
kuweka taarifa muhimu za wanafunzi
katika Mkoa husika.
(b) Itafanya mikutano yake ya kawaida mara mbili
kila muhula wa masomo, lakini itaweza
kufanya mkutano usio wa kawaida wakati
wowote.
(c) Kuandaa shughuli za vikao vyote vya juu yake.
(d) Katibu wa Seneti wa Shirikisho la Mkoa
ataongoza mikutano ya Kamati ya Uratibu ya
Mkoa lakini kama hayupo, atateuliwa mjumbe
mmoja kutoka miongoni mwao kuongoza kwa
muda.
19 | P a g e “ e l i m u n a m a e n d e l e o y a w a t u ”
Ibara ya 33
Viongozi wa
Shirikisho la
Mkoa
Kutakuwa na viongozi wa Shirikisho la Mkoa kama
ifuatavyo:-
i. Mwenyekiti wa Seneti wa Shirikisho la Mkoa
ii. Katibu wa Seneti wa Shirikisho la Mkoa
Ibara ya 34
Mwenyekiti wa
Seneti wa
Shirikisho la
Mkoa
(a) Mwenyekiti wa Seneti wa Shirikisho la Mkoa
wa vyuo vya elimu ya juu atachaguliwa na
Mkutano Mkuu wa Seneti wa Shirikisho la
Mkoa na atakuwa katika nafasi hiyo kwa
mujibu wa Ibara ya 16 ya Kanuni hizi.
(b) Mwenyekiti atakuwa na kazi kama ilivyoelezwa
katika Katiba ya CCM ibara ya 99 (2) na (4).
Ibara ya 35
Katibu wa Seneti
wa Shirikisho la
Mkoa
(a) Katibu wa Seneti wa Shirikisho la Mkoa
atachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Seneti wa
Shirikisho la Mkoa na atakuwa katika nafasi
hiyo kwa mujibu wa Ibara ya 16 ya Kanuni
hizi.
(b) Katibu wa Seneti wa Shirikisho la Mkoa
atakuwa na majukumu yafuatayo:
i. Kuratibu kazi zote za CCM katika
Shirikisho la Mkoa.
ii. Kusimamia kazi za uendeshaji wa Chama
katika Shirikisho la Mkoa.
iii. Kufuatilia na kuratibu masuala ya
uzalendo,maadili ya Taifa,elimu ya
kujitegemea,uongozi na utafiti.
iv.
v. Kuratibu shughuli za uchaguzi wa
viongozi wa Matawi ya Chama katika
Shirikisho la Mkoa.
Ibara ya 36
Vikao vya
Shirikisho la
Taifa.
Ibara ya 37
Mkutano Mkuu
wa Shirikisho la
Taifa.
FUNGU LA TATU- VIKAO VYA SHIRIKISHO LA
TAIFA
Kutakuwa na vikao vifuatavyo katika ngazi ya Taifa:
i. Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Taifa.
ii. Kamati ya Uratibu ya Shirikisho la Taifa.
(a) Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Shirikisho la
Taifa ambao utakuwa na wajumbe wafuatao:
i. Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu Tanzania
ii. Makamu wa Mwenyekiti wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
iii. Katibu Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
iv. Katibu wa Siasa na Uenezi wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
v. Katibu wa Uchumi na Fedha wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
vi. Katibu wa Uhamasishaji wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
vii. Mlezi wa Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya
elimu ya juu (ambaye hatashiriki kupiga kura
katika Kikao chochote).
viii. Wajumbe watatu wa Halmashauri Kuu ya
CCM ya Taifa kutoka Shirikisho la Wanafunzi
wa vyuo vya elimu ya juu (mmoja kutoka
Tanzania Zanzibar na wawili kutoka Tanzania
Bara).
ix. Wenyeviti wote wa Seneti wa Shirikisho la
Mikoa
x. Makatibu wote Seneti wa Shirikisho la Mikoa.
xi. Makatibu wote wa Siasa na Uenezi wa Seneti
wa Shirikisho la Mikoa.
xii. Makatibu wote wa Uchumi na Fedha wa
Ibara ya 38
Kazi za
Mkutano Mkuu
wa Shirikisho la
Taifa.
Seneti wa Shirikisho la Mikoa.
xiii. Makatibu wote wa Uhamasishaji wa Seneti wa
Shirikisho la Mikoa.
xiv. Wajumbe wote wa Kamati ya Uratibu ya
Shirikisho la Mikoa.
xv. Viongozi Wakuu wote wa CCM wa Tawi
xvi. Wenyeviti wote wa kila Jumuiya ya Wananchi
inayoongozwa na CCM katika Matawi ya vyuo
vya elimu ya juu nchini.
(b) Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Taifa ndicho
kikao kikuu cha Shirikisho la wanafunzi wa vyuo
vya elimu ya juu nchini.
(c) Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Taifa utafanyika
mara moja kila baada ya miaka mitatu au
inapohitajika kufanyika.
(d) Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo
vya elimu ya juu Tanzania ataoongoza Mkutano
Mkuu wa Shirikisho la Taifa kama hayupo
Makamu wa Mwenyekiti ataoongoza.
Kazi za Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Taifa
zitakuwa kama ifuatavyo:
(a) Kupokea na kujadili taarifa za kazi
zilizotolewa na Kamati ya Uratibu ya
Shirikisho la Taifa na kutoa maelekezo ya
utekelezaji wa Siasa kwa kipindi kijacho.
(b) Utajadili mambo yote muhimu ya
wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
kuhusu uzalendo na maadili ya
Taifa,elimu ya kujitegemea,
uwezeshaji,mikopo ya elimu ya
juu,ubunifu na uongozi. Aidha,kutoa
mapendekezo kwa vikao vya juu kadri
inavyolazimu.
(c) Kuhakikisha kwamba maazimio na
maagizo ya ngazi ya Taifa yanatekelezwa
ipasavyo.
(d) Kuwa kiungo kati ya Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na
vikao vya Chama vya kitaifa kupitia
Sekretariet ya Halmashauri Kuu ya CCM
ya Taifa.
(e) Aidha,unapofika wakati wa Uchaguzi
Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Taifa
utashughulikia mambo yafuatayo:
i. Kuratibu shughuli za Uchaguzi wa
Viongozi katika Shirikisho la Taifa
na Uchaguzi wa Uwakilishi kupitia
vyombo vya dola.
ii. Utamchagua Mwenyekiti wa
Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo
vya elimu ya juu Taifa,Makamu wa
Mwenyekiti Taifa,Katibu wa Siasa
na Uenezi Taifa,Katibu wa Uchumi
na Fedha Taifa,Katibu wa
Uhamasishaji Taifa,na Wajumbe
watatu wa Halmashauri Kuu ya
CCM ya Taifa. Aidha,Viongozi hao
wote watashika nafasi zao za
uongozi kwa mujibu wa ibara ya 16
ya Kanuni hizi.
(f) Kuunda Kamati Mbalimbali kadri
itakavyoonekana inafaa.
(g) Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi
wa vyuo vya elimu ya juu Taifa
ataoongoza Mkutano Mkuu wa Shirikisho
la Taifa,na kama hayupo Makamu wa
Mwenyekiti Taifa ataoongoza.
(h) Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Taifa wa
Ibara ya 39
Kamati ya
Uratibu ya
Shirikisho la
Taifa.
kawaida utafanyika kila baada ya miaka
mitatu. Lakini unaweza kufanyika wakati
wowote iwapo itaonekana inafaa.
(a) Kutakuwa na Kamati ya Uratibu ya
Shirikisho la Taifa ambayo itakuwa na
wajumbe wafuatao:
i. Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi
wa vyuo vya elimu ya juu Taifa
ii. Makamu wa Mwenyekiti wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
Taifa
iii. Katibu Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
iv. Katibu wa Siasa na Uenezi wa Shirikisho
la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
Taifa
v. Katibu wa Uchumi na Fedha wa
Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya
elimu ya juu Taifa
vi. Katibu wa Uhamasishaji wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
Taifa
vii. Wajumbe kumi walioteuliwa na
Sekretariet ya Halmashauri Kuu ya CCM
ya Taifa.
(b) Kamati ya Uratibu ya Shirikisho la Taifa
itafanya mikutano yake ya kawaida mara
moja kila muhula wa masomo.
(c) Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu ataongoza mikutano
yote ya Kamati ya Uratibu ya Shirikisho la
Taifa na kama hayupo Makamu wa
Mwenyekiti ataongoza.
Ibara ya 40
Kazi za Kamati
ya Uratibu ya
Shirikisho la
Taifa.
Ibara ya 41
Viongozi wa
Shirikisho la
Wanafunzi wa
vyuo vya elimu
ya juu Taifa.
Kazi za Kamati ya Uratibu ya Shirikisho la Taifa
zitakuwa kama ifuatavyo:
i. Kutoa uongozi wa Siasa katika Shirikisho
la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
nchini.
ii. Kusimamia utekelezaji wa shughuli za
kila siku za Shirikisho la wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya nchini.
iii. Kuratibu masuala ya fedha,rasilimali
watu,na vitendea kazi ili kufanikisha
malengo yaliyowekwa.
iv. Kutoa ufafanuzi wa masuala ya kijamii
kuhusiana na mazingira na wakati.
v. Kutengeneza mfumo wa kiutendaji wa
kitaasisi kwa kufikia malengo yake,aidha
kwa mtendaji mmoja mmoja au kwa
pamoja.
vi. Kuweka kipaumbele katika masuala ya
misingi ya Shirikisho kama
vile,kupanga,kuratibu, kusimamia
utekelezaji na kupima matokeo ya kazi.
vii. Kusimamia tafiti ili kukisaidia chama
kufahamu changamoto zake na kujua
tathimini ya utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi.
Kutakuwa na Viongozi wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Taifa
kama ifuatavyo:
i. Mwenyekiti wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
Taifa
ii. Makamu wa Mwenyekiti wa Shirikisho
la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya
juu Taifa
iii. Katibu Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la
Ibara ya 42
Upatikanaji wa
Viongozi wa
Shirikisho la
Wanafunzi wa
vyuo vya elimu
ya juu Taifa.
Ibara ya 43
Mwenyekiti wa
Shirikisho la
Wanafunzi wa
vyuo vya elimu
ya juu Taifa.
Ibara ya 44
Makamu wa
Mwenyekiti wa
Shirikisho la
Wanafunzi wa
vyuo vya elimu
ya juu
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
iv. Mwenyekiti wa Taifa,Makamu wa
Mwenyekiti wa Taifa na Katibu
Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
watakuwa wajumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM ya Taifa.
Endapo Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu Taifa atatoka Tanzania
Bara,Makamu wa Mwenyekiti Taifa atatoka
Tanzania Zanzibar au kinyume chake.
(a) Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu Taifa atachaguliwa
na Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Taifa na
atakuwa katika nafasi hiyo kwa mujibu wa
Ibara ya 16 ya Kanuni hizi.
(b) Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu Taifa atakuwa na
kazi kama ilivyoelezwa katika Katiba ya
CCM ya mwaka 1977 ibara ya 99 (2) na
(4).
(a) Makamu wa Mwenyekiti wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Taifa
atachaguliwa na Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Taifa na atakuwa katika nafasi
hiyo kwa mujibu wa Ibara ya 16 ya Kanuni
hizi.
(b) Makamu wa Mwenyekiti wa Shirikisho la
wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Taifa
atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa
Ibara ya 45
Katibu Mtendaji
Mkuu wa
Shirikisho la
Wanafunzi wa
vyuo vya elimu
ya juu.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu Taifa na atafanya
kazi zote za Shirikisho la Wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu atakazopewa na
Mwenyekiti wa Shirikisho la wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu Taifa.
(a) Katibu Mtendaji Mkuu wa Shirikisho
la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya
juu atateuliwa na Halmashauri Kuu
ya CCM ya Taifa.
(b) Atakuwa Mtendaji Mkuu wa shughuli
zote za CCM katika Shirikisho la
wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
na atafanya kazi chini ya uongozi
wa Kamati ya Uratibu ya Shirikisho
la Taifa.
(c) Majukumu yake ni haya yafuatayo:-
i. Kuratibu kazi zote za Shirikisho
na kuchukua hatua za
utekelezaji wa maamuzi yake.
ii. Kusimamia kazi za Utawala na
Uendeshaji wa Chama katika
Shirikisho.
iii. Kufuatilia na kuratibu masuala
ya Usalama na Maadili ya
Chama katika Shirikisho.
iv. Kusimamia udhibiti wa fedha na
mali ya Shirikisho.
v. Ataitisha mikutano ya Kamati
ya Uratibu ya Shirikisho la Taifa
na Mkutano Mkuu wa Shirikisho
la Taifa,baada ya kushauriana
na Mwenyekiti wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu
ya juu Taifa.
vi. Atakuwa ndiye Mkurugenzi wa
Ibara ya 46
Viongozi
wengine wa
Shirikisho la
Wanafunzi wa
vyuo vya elimu
ya juu Taifa.
Ibara ya 47
Katibu wa Idara
ya Nje na
Uhusiano wa
Kimataifa.
Ibara ya 48
Katibu wa Idara
ya Uwezeshaji.
Uchaguzi katika Shirikisho na
kusimamia masuala yote ya
Shirikisho.
vii. Atakuwa Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
viii. Kuwa kiungo kati ya
Shirikisho na vikao vya Chama
Kitaifa kupitia Sekretarieti ya
Halmashauri Kuu ya Taifa,na
kuwa Mjumbe wa Sekretariet ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Kutakuwa na viongozi wengine wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Kitaifa kama
ifuatavyo:
i. Katibu wa Idara ya Nje na Uhusiano wa
Kimataifa.
ii. Katibu wa Idara ya Uwezeshaji.
iii. Katibu wa Idara ya Elimu,Utafiti na Uongozi.
(a) Katibu wa Idara ya Nje na Uhusiano wa
Kimataifa atateuliwa na Kamati ya Uratibu
ya Shirikisho la Taifa.
(b) Atakuwa ndiye Msimamizi Mkuu wa mambo
ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ndani ya
Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu
ya juu kwa mujibu wa Kanuni hizi.
(c) Atashughulikia masuala ya kuimarisha
mahusiano na taasisi za wanafunzi za
kitaifa na kimataifa.
(a) Katibu wa Idara ya Uwezeshaji atateuliwa
na Kamati ya Uratibu ya Shirikisho la Taifa.
(b) Atakuwa ndiye Msimamizi Mkuu wa
masuala ya uwezeshaji kwa wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu.
Ibara ya 49
Katibu wa Idara
ya Elimu,Utafiti
na Uongozi.
Ibara ya 50
Watendaji wa
Shirikisho la
Wanafunzi wa
vyuo vya elimu
ya juu.
(c) Ataratibu semina na midahalo inayohusu
ajira,kujiajiri na uwezeshaji na kutoa fursa
ambazo wanafunzi watanufaika na ujuzi
huo.
(a) Katibu wa Idara ya Elimu,Utafiti na Uongozi
atateuliwa na Kamati ya Uratibu ya
Shirikisho la Taifa.
(b) Atakuwa ndiye Msimamizi Mkuu wa
masuala yanayohusu elimu,utafiti na
uongozi.
(c) Atawatumia makada wasomi kwa ajili ya
kuleta mabadiliko ya mawazo na fikra mpya
ikiwa ni pamoja na kushauri kwa kutumia
tafiti mbalimbali kwa maslahi ya Chama na
Taifa kwa ujumla.
(d) Atajenga mtazamo chanya juu ya elimu ya
kujitegemea kwa vijana na kuwakuza katika
ustadi wa kujiajiri kwa maendeleo ya Taifa.
SEHEMU YA NNE- WATENDAJI WA
SHIRIKISHO LA WANAFUNZI WA VYUO VYA
ELIMU YA JUU
Kutakuwa na watendaji wa Shirikisho la wanafunzi
wa vyuo vya elimu ya juu wafuatao:
(a) Katibu Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la
wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
(b) Makatibu wa Idara
(c) Makatibu wa Shirikisho la wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu wa Makao Makuu.
(d) Makatibu wa Shirikisho la Mikoa
(e) Makatibu wa Matawi
Ibara ya 51
Makatibu wa
Shirikisho la
Wanafunzi wa
vyuo vya elimu
ya juu.
Ibara ya 52
Idara za
Shirikisho la
Wanafunzi wa
vyuo vya elimu
ya juu.
Ibara ya 53
Mlezi wa
Shirikisho la
Wanafunzi wa
vyuo vya elimu
ya juu Taifa.
(a) Kutakuwa na Makatibu wa Shirikisho la
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wa
Makao Makuu,Mikoa,na Matawi.
i. Makatibu wa Shirikisho la Wanafunzi
wa vyuo vya elimu ya juu wa Makao
Makuu watateuliwa na Sekretarieti ya
Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.
ii. Makatibu wa Shirikisho la Wanafunzi
wa vyuo vya elimu ya juu wa
Shirikisho la Mikoa watachaguliwa na
Mkutano Mkuu wa Seneti wa
Shirikisho la Mkoa.
iii. Makatibu wa Shirikisho la Wanafunzi
wa vyuo vya elimu ya juu wa Matawi
watachaguliwa na Mkutano wa
Halmashauri Kuu ya Tawi.
SEHEMU YA TANO – IDARA ZA SHIRIKISHO
LA WANAFUNZI WA VYUO VYA ELIMU YA JUU
Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
utakuwa na Idara zifuatazo:
i. Idara ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa.
ii. Idara ya Uwezeshaji.
iii. Idara ya Elimu,Utafiti na Uongozi.
SEHEMU YA SITA - MENGINEYO
Kutakuwepo na Mlezi wa Shirikisho la Wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu ambaye atateuliwa na Kamati
Kuu ya Halmashauri ya CCM ya Taifa.
Ibara ya 54
Mlezi wa
Shirikisho la
Mkoa.
Ibara ya 55
Mlezi wa Tawi.
Ibara ya 56
Akidi ya Vikao.
Ibara ya 57
Kiwango cha
kufikia uamuzi.
Ibara ya 58
Nafasi zikiwa
wazi.
Kutakuwepo na Mlezi wa Shirikisho la Mkoa ambaye
atateuliwa na Mkutano Mkuu wa Seneti wa Mkoa.
Kutakuwepo na Mlezi wa Tawi ambaye atateuliwa
na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Tawi.
Isipokuwa kama imeagizwa vinginevyo katika
Kanuni hizi kiwango cha Mikutano ya Vikao vyote
vya Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya
juu kitakuwa zaidi ya nusu ya wajumbe walio na
haki ya kuhudhuria katika kikao kinachohusika.
Katika masuala yanayohusu Shirikisho la Wanafunzi
wa vyuo vya elimu ya juu au jambo lingine lolote
linalohusu kubadilisha utaratibu wowote wa kimsingi
katika Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Taifa uamuzi
utakuwa kwa makubaliano ya theluthi mbili ya
wajumbe kutoka Tanzania Zanzibar na theluhti mbili
kutoka Tanzania Bara.
Wakati wowote kunapotokea nafasi miongoni mwa
viti vyovyote vya Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo
vya elimu ya juu,vikao ya ngazi zinazohusika
yatajaza nafasi hizo.
Ibara ya 59
Mahudhurio
katika Mkutano.
Ibara ya 60
Mapato ya
Shirikisho la
Wanafunzi wa
vyuo vya elimu
ya juu.
Ibara ya 61
Tafsiri
Mjumbe yeyote wa kikao chochote kilichowekwa na
Kanuni hizi ataacha kuwa Mjumbe wa kikao hicho
iwapo hatahudhuria Mikutano mitatu ya Kikao
kinachomhusu,isipokuwa kwa sababu zinazokubalika
na Kikao chenyewe.
Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
utakuwa na mapato kutokana na kiingilio na ada za
wanachama wake pamoja na mapato mengine
yanayotokana na shughuli mbalimbali pamoja na
fedha ya hiari iliyochangishwa kwa madhumuni
yoyote maalum yatakayokubalika na Vikao.
Kwa mujibu wa muongozo huu maneno yafuatayo
yatakuwa na maana kama yalivyoelezwa hapa chini:
i. Tawi: Inamaanisha ni Tawi la CCM la
Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya
juu.
ii. Shirikisho la Mkoa: Ni muungano wa matawi
ya Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu
ya juu ambayo yapo katika Mkoa husika.
iii. Shirikisho la Taifa: Ni muungano wa Shirikisho
la Mikoa la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya
juu.
iv. Katiba : Inamaanisha ni Katiba ya Chama Cha
Mapinduzi ya Mwaka 1977
v. Seneti: Ni Mkutano Mkuu wa Shirikisho la

Post a Comment