Kitendawili cha tarehe rasmi ya Watanzania kupiga Kura ya Maoni itakayopitisha au kukwamisha Katiba Inayopendekezwa, kitateguliwa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(Nec) baada ya kukamilisha uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapigakura Aprili mwaka ujao.
Nec imebainisha hayo jijini Dar es Salaam jana ikieleza kuwa tayari Serikali imetoa Sh15 bilioni za uboreshaji huo na kwamba utakamilika Serikali itakamilisha kutoa Sh270 bilioni zinazohitajika kwa ajili ya uboreshaji wa daftari hilo.
Hadi sasa, kuna mkanganyiko kuhusu tarehe hiyo baada ya Rais Jakaya Kikwete kutaja mwezi Aprili mwakani kama wakati wa kupiga kura hiyo, akipingana na Machi 15 iliyotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema.
Makamu mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa tume hiyo itakamilisha daftari hilo ifikapo Aprili mwakani.
‘’Mpaka sasa Serikali imeshatoa Sh15 bilioni, tutaendelea kupokea kidogo kidogo kutoka Hazina. Ikiwa zikifika kwa wakati, tutakamilisha zoezi hili Aprili 18 mwakani,’’ alisema na kuongeza:
‘’Mtakumbuka awali tuliarifu wananchi kuwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura lingeanza Septemba mwaka huu, hata hivyo halikuanza kutokana na kuchelewa kupatikana kwa fedha kutoka serikalini.’’
‘’Mtakumbuka awali tuliarifu wananchi kuwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura lingeanza Septemba mwaka huu, hata hivyo halikuanza kutokana na kuchelewa kupatikana kwa fedha kutoka serikalini.’’
Alisema kuwa kwa sasa Nec imeanza kupewa fedha na Serikali kuwawezesha kuanza kwa zoezi hilo la uboreshaji daftari hilo.
Jaji Hamid aliongeza kwamba mara baada kupokea kiasi hicho pamoja na vifaa vya uboreshaji wa daftari hilo, Nec ilianza kutoa mafunzo kwa watendaji wake.
“Novemba mwaka huu, tutafanya majaribio ya uboreshaji daftari la wapigakura kutumia mfumo wa ‘Biometric Voter Registration’ katika majimbo matatu ya uchaguzi ya Kawe Manispaa ya Kinondoni, Halmashauri ya Mji wa Kilombero na Mlele Halmashauri ya Mji wa Katavi,” alisema.
Post a Comment