*NI ALIYEPEWA TENDA NA CHADEMA KUJENGA MNARA WA MAREHEMU MWANGOSI
*ADAI CHADEMA ILIMTALIPELI ITAMLIPA KWA KAZI HIYO LAKINI HADI SASA PATUPU
*ANG'OKA CHADEMA NA VIJANA 27
Katibu
wa Chadema Kata ya Igowole, wilayani Mufindi mkoani Iringa, Josephat
Soda akitangaza kukihama chama hicho, mbele ya maelfu ya wananchi katika
mkutano wa hadhara wa Kinana uliofanyika leo, Oktoba 10, 2014, kwenye
mjini mdogo wa Nyololo. Soda amesema ameamua kukihama chama hicho baada
ya kubaini kuwa ni matapeli waliompa kazi ya kujenga mnara wa kumbukumbu
wa mwandishi wa habari David Mwangosi, aliyeuawa katika mapambano cha
Chadema na Polisi wakati wa maandamano yaliyofanywa na chama hicho mwaka
juzi katika mji huo mdogo wa Nyololo ambapo aliujenga mnara huo wa
gharama zake na kukopa saruji kwa ahadi ya kulipwa na viongozi wa
Chadema lakini hadi leo ameambilia patupu.
Soda
akikabidhi kadi yake ya Chadema kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana baada ya uamuzi wake wa kuamua kuhamia CCM kwenye mkutano huo.
Kinana akionyesha kadi ya Soda na vijana wengine 27 waliohamia CCM kumfuata Soda
Soda
akizungumza mbele ya Kinana. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenzi
nape Nnauye aliyefanyakazi ya kumkaribisha Soda jukwaani.
Vijana walioamua kumfuata Soda kuhamia CCM wakionysha kadi zao za Chadema kabla ya kumkabidhi Kinana
Kinana akimkabidhi Soda kadi ya CCM. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iriga, Jesca Msambatavangu
Kadi mpta ya CCM aliyokadhiwa Soda
Vijana waliomfuata Soda kuhamia CCM wakipewa kadi za CCM na Kinana
Wananchi wakishangilia baada ya Kinana kumpokea Soda na vijana hao
Soda (kulia) akiungana na wenzake kula kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za CCM na Kinana
Baadhi
ya waandishi wa habari walioko kwenye msafara wa Kinana mkoani Iringa,
wakiwa kwenye mnara uliojengwa na Soda kwa ajili ya kumbukumbu ya
Mwangosi. Hata hivyo mnara huo hauna maandishi wala chochote
kinachoonyesha kuwa umanhusu marehemu Mwangosi
Kiongozi
wa bendi ya CCM ya Mafinga, akiongoza kuimba wimbo maalum wa CCM
inavyotekelza ilani ya Uchaguzi, wakati wa mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana (kulia) akiungana na wananchi kuselebuka wimbo huo maakum wa CCM
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na wanamuzi wa bendi hiyo ya CCM baada ya wimbo huo
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na Nape wakiitazama albamu ya wimbo huo maalum wa CCM. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog
Post a Comment